Baada ya kutumikia adhabu ya kutohudhuria vikao vitano vya Bunge, wabunge watano wa (Chadema), warejea kwa ari Bungeni . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, April 30, 2013

Baada ya kutumikia adhabu ya kutohudhuria vikao vitano vya Bunge, wabunge watano wa (Chadema), warejea kwa ari Bungeni .



Mchungaji Peter Msigwa.
Baada ya kutumikia adhabu ya kutohudhuria vikao vitano vya Bunge, wabunge watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana (April 29,2013) waliingia bungeni wakionekana kuwa na ari mpya. 



Wabunge waliosimamishwa Aprili 17,2013  ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.



Wengine ni Highness Kiwia (Ilemela), Ezekiel Wenje (Nyamagana), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Mbeya Mjini) na Godbless Lema (Arusha Mjini). 



Jana asubuhi Mchungaji Msigwa alikuwa miongoni mwa wabunge waliowahi kuingia mapema ndani ya Ukumbi wa Bunge na kufuatiwa na Lissu muda mfupi baada ya kikao kuanza. 



Ndani ya Ukumbi wa Bunge, Msigwa alipata nafasi ya kuuliza swali namba 115 lililokuwa liulizwe na Joyce Mukya kuhusu Kampuni ya Kamwene Woodworks .

Godbless Lema
Kwa upande wake, Lissu aliomba mwongozo wa Spika kuhusu kukwama kwa Bajeti ya Wizara ya Maji. 



Wabunge wengine haikujulikana sababu za kutofika jana licha ya kuwa adhabu yao ilikwisha tangu April 25 huku taarifa zikieleza kuwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema alikuwa kapelekwa mahakamani kujibu staka la uchochezi.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad