![]() |
Mtoto
huyu alipewa
jina
la 59 anaendelea
kupokea
matibabu.
|
Mtoto
mchanga aliyeokolewa kutoka ndani ya bomba la maji taka nchini China, alianguka
ndani ya bomba hilo kwa bahati mbaya,kwa Mujibu wa Mama yake mtoto huyo
amesema.
Mama huyo
ambaye bado hajatajwa jila lake, aliwambia Polisi kuwa alijifungua Mwanawe
akiwa chooni na kuwa mtoto huyo aliteleza na kuanguka ndani ya bomba hilo kwa
bahati mbaya.
Mama huyo
anaripotiwa kuangua kilio cha Kumpoteza mwanawe , licha ya kuwa Mwanzoni hakukubali kuwa ni mwanawe hadi baadaye.
Mtoto huyo
anapatiwa matibabu hospitalini baada ya
kuokolewa kutoka ndani ya bomba la maji taka.
Bomba hilo
lilikatwa kwa ustadi baada ya majirani kusikilia kilio cha mtoto huyo mjini
Jinhua Jumamosi(May 26,2013).
Shirika la
habari la Zhezhong, lilisema kuwa mama yake mtoto huyo mwenye umri wa miaka 22,
aliwambia Polisi kuwa hangeweza kumudu gharama ya kulea mimba kwa Sababu Hajaolewa
na aliiweka mimba yake kuwa siri kubwa.
![]() |
Mtoto huyu
alipewa jina la 59 anaendelea kupokea matibabu.
|
Alisema kuwa
alijaribu kumzuia mtoto wake kuanguka baada ya kujifungua kwa ajali akiwa
hospitalini lakini alianguka ndani ya bomba.
Hata hivyo
alimweleza mpangaji wake kulingana na shirika la habari la Xinhua.
Mama huyo
alisema hakuwa na uwezo wa kumlea mwanawe kwa hivyo hakumwambia yeyote kuwa ni
mwanawe.
Hata hivyo
baadaye alijitambulisha na kuwambia Polisi ni mwanawe baada ya kuokolewa kwake.
Polisi
wanachunguza ikiwa tukio hilo lilikuwa la ajali au kilikuliwa kitendo cha makusudi.
Mtoto huyo
alipatikana ndani ya bomba lenye urefu wa nchi nne na alipata majeraha madogo
kichwani na mikononi lakini anaendea kupata matibabu.
Kisa hicho
kimezua mjadala mkali kwenye mitandao ya China huku baadhi wakisema kuwa mtoto
huyo alikuwa ametupwa na mama yake kwa makusudi.
Sheria za
China za kupanga uzazi ni kali mno huku familia ikiruhisiwa kuzaa mtoto mmoja
pekee na wazazi wanaweza kuadhibiwa kwa kutozwa faini ikiwa watapatikana na
hatia ya kupata zaidi ya mtoto mmoja.
No comments:
Post a Comment