Marehemu`Ngwair’(28).
|
Wakati
mazishi ya mwanamuziki marehemu Albert Mangwea(28) maarufu kama `Ngwair’
yakitarajiwa kufanyika mjini Morogoro, maeneo ya Kihonda baada ya mwili
kuwasili nchini, hospitali iliyomfanyia vipimo imethibitisha kuwa pombe na dawa
za kulevya kupita kiasi ndivyo vilivyomuua.
Mwili wa
mwanamuziki huyo, ambaye alitamba kwenye miaka ya 2000 na wimbo wa `Mikasi’,
unatazamiwa kuletwa kesho nchini na kuagwa Jumamosi kabla ya kusafirishwa
kwenda kwao Kihonda, Morogoro kwa mazishi.
Kwa mujibu
wa taarifa Mangwea alifariki dunia juzi kwenye Hospitali ya St Hellen, iliyopo
Johannesburg, Afrika Kusini alikokuwa amekwenda kwa shughuli za muziki.
Ripoti
iliyochapwa na mitandao mbalimbali ya ndani na nje ya nchi inasema marehemu
alifikwa na umauti baada ya kulewa kupindukia, kibaya zaidi alikuwa hajala.
Siku ya kifo
chake, Mangwea alianguka nyumbani kwa rafiki zake akiwa katika hali hiyo ya
kulewa sana.
Kwa mujibu
wa ripoti hiyo, baada ya kufikishwa hospitalini, Mangwea aligundulika kulewa
mara tano ya kipimo cha kilevi kilichopitishwa na serikali ya Afrika ya Kusini,
ambacho ni 416mg za pombe kwenye kila milimita 100(kwa mlevi anayeendesha
chombo cha moto).
Pia marehemu
alikutwa na upungufu wa hewa ya oksijeni kwenye seli na tishu za mwili wake.
![]() |
Hospitali ya St Hellen. |
Ripoti hiyo
ilibainisha kuwa Mangwea, maarufu Ngwair, alikuwa na tatizo la kutokula chakula
vizuri kabla ya kifo chake na pia kukosa muda wa kupumzika.
Sampuli
zilizopatikana mwilini mwake zinaonyesha mkusanyiko wa dawa za kulevya
mbalimbali zikiwemo heroine, cocaine chafu na bangi ya gramu 0.08 ambavyo vilikutwa
kwenye damu yake.
Kifo chake
kilitokana na mshtuko wa moyo na kushindwa kupumua, hali iliyosababisha mapigo
ya moyo wake kusimama kwa sekunde chache, na kusababisha kifo chake.
Mwili wa
Ngwair ulionekana kana kwamba alitokwa na damu nyingi puani baada ya kuonyeshwa
kwa Watanzania wengi jana jioni Johannesburg, Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment