Wananchi wakiangalia mwili wa aliyekuwa Mfanyabiashara wa katika moja ya
maduka ya Kariakoo aliyetambulika kwa jina moja la Shirima, aliyejirusha kutoka
ghorofa ya 9 ya Hoteli ya Concord ni leo mchana(03,May,2013) huu maeneo ya Kariakoo.
Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea, wameeleza kuwa walipatwa na mshuko
mkubwa baada ya kusikika kishindo cha kitu kilichoangua na kuhisi labda ni 'yale
yale' ya maghorofa kuporomoka yenyewe baada ya kuguswa na Kunguru, kumbe ni mtu
huyo aliyeanguja juu gari hilo.
Na baada ya watu hao kusogea eneo hilo walikuta ni mwili wa mtu
aliyeanguka kutoa ghorofani ambaye baadhi yao waliweza kumtambua kwa jina moja
kuwa ni Shirima. Baada ya tukio hilo wasamaria wema wamemkimbiza mtu huyo
hospitali kutokana na kwamba alikuwa bado akipumua.
Mfanyabiashara huyo alijirusha toka ghorofani na kuangukia juu ya Gari
aina ya Toyota Corolla ambayo ni taxi iliyokuwa imeegeshwa nje ya hoteli hiyo.
Haikuweza kufahamika chanzo cha jamaa huyo kujirusha kutoka ghorofani. Picha
kwa hisani ya Mtaa kwa Mtaa. Kwa hisani ya Sufiani Mafoto.
No comments:
Post a Comment