Bw.William
Lukuvi.
|
Hatimaye
Serikali imefuta matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka 2012 kufuatia
asilimia 65.5 ya Wanafunzi wote waliofanya mtihani huo kupata daraja sifuri na
kupelekea kuundwa kwa Tume ya Taifa ya kuchunguza suala hilo.
Akitoa kauli
ya Serikali Bungeni kuhusu taarifa ya awali ya tume hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais Uratibu na Bunge WILLIAM LUKUVI amesema, kiwango cha ufaulu kimeanza
kushuka mwaka 2008 kuliko miaka iliyotangulia.
Kufuatia
mapendekezo ya Tume ya Taifa ya kuchunguza matokeo hayo, tayari Baraza la
Mawaziri limeridhia uamuzi huo na kutaka mapendekezo yote ya tume hiyo yaanze
kutekelezwa mara moja.
Tume hiyo,
ilipewa hadidu za rejea kadhaa ikiwemo kutafuta sababu za matokeo mabaya ya
Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012; Kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha
ufaulu katika mitihani ya Kidato cha Nne mwaka 2011 hadi 2012.
Kutoa
mapendekezo ya hatua za kuchukua kukabiliana na tatizo la mwenendo wa kushuka
kwa kiwango cha elimu mara moja,kipindi cha muda mfupi, kati na kipindi cha
muda mrefu.
Pia Tume
hiyo ilipewa jukumu la kutathmini nafasi ya Halmashauri katika kusimamia Elimu
ya Sekondari katika Halmashauri zake na
kuanisha sababu nyingine zinazoweza kuwa zimechangia hali hii ya matokeo.
BungeniDodoma. |
Uchambuzi wa
taarifa hiyo ya awali unaonyesha kuwa kutokana na uchunguzi uliofanyika, kwa
muhtasari, Tume imebaini mambo muhimu kadhaa kama vile matokeo ya Kidato cha
Nne kuanzia mwaka 2008 kuendelea kushuka kuliko miaka iliyotangulia kwa sababu
mbalimbali ikiwemo changamoto zinazotokana na mafanikio yaliyopo sasa ya
kuongezeka sana kwa Idadi ya Shule za Msingi na za Sekondari,hasa kati ya mwaka
2001 na 2013; na hivyo kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliopo Shuleni.
Kwa mfano,
katika kipindi cha mwaka 1961 hadi 2001 Idadi ya Wanafunzi wa Shule za Msingi
imeongezeka kutoka Wanafunzi 486,470(1961) hadi 4,875,764 mwaka 2001, sawa na
ongezeko la Wanafunzi 4,389,294.
katika
kipindi hicho cha takriban miaka 40.
Hata hivyo,
ongezeko hilo haliendani na mazingira ya kufundishia na kujifunzia, ikiwemo
upungufu wa miundombinu muhimu ya shule kama vile madarasa,maabara, madawati,
maktaba, nyumba za walimu, hosteli na majengo mengine muhimu ya shule.
Vilevile, kuna tatizo la uhaba wa walimu,vitabu, zana za kufundishia na
matatizo ya ukaguzi wa shule.
Tume
imebaini pia kwamba, pamoja na Wanafunzi hawa kuwa katika mazingira
yanayofanana na ya wenzao wa miaka iliyopita na kwamba ufanisi katika shule kwa
ujumla umekuwa unashuka kwa sababu mbalimbali,zikiwemo za mabadiliko ya
mchakato wa kuandaa na kutoa matokeo ya mtihani kwa mwaka 2012.
Mfumo
uliotumika mwaka 2012 katika kupanga matokeo na madaraja ni tofauti na ule
uliotumika mwaka 2011 na miaka iliyotangulia.
Hata hivyo
baadhi ya wadau wa elimu, wazazi na wanafunzi wamehoji uamuzi huo wa serikali
kama hautakuwa na athari kwa wanafunzi waliofaulu na kujiandaa na masomo ya
kidato cha tano na wale ambao tayari wamejiandikisha kurudia mitihani yao kwa
njia ya kulipia.
Kati ya
wanafunzi 367,756 waliofanya Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2012 watahiniwa
126,847 walifaulu ambapo 23, 520 pekee ndio waliopata daraja la kwanza hadi la
tatu.
No comments:
Post a Comment