Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ na mumewe, Gardner G. Habashi. |
Watu
wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi
itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi Na bado naendelea ku experience mambo magumu
zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.
Siku za
karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki
umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki.
Wanaomiliki chombo cha habari.
Nasimama na
kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha
nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.
Watu hao
ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada
ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila
kuburuzwa.
Wanapita
kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni
kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive
bila wao.
Mimi ni
msanii tofauti na hao mnaofikiria.
Nadhani
mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate,
na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda
Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo
ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.
Nita survive
kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.Wakati bado
wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza
kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.
Na huu ndio
wosia wangu kwa watu hao.
‘Lady Jaydee’ |
Natambua
wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu
alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Ila naomba
nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee
lolote kuhusiana na kifo changu.
Ruge
Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige mame,Enyi
mtakaokuwa hai baada yangu.
Kama
wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai,Hakuna haja
ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja
wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao
wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.
Niliamua
kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu
wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo
yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth
Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia
fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.
Na hii ni
kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi
kumiliki dunia..Kama mnasema
mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi
nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe
star..
Kwa roho
zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.Talent
haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina
Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.
Mnawatishia
wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne
mmeshakaa kunijadili.Mnadhani je!
nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi??
nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa
ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani??Kwahiyo
mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??
Ilikuwa
niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake
ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.
Kila siku
mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu
hamjui tu.
Mtu hela
zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma??Roho gani
hiyo??
Naishia hapo
na sitabatilisha kauli yangu.
JIDE.
No comments:
Post a Comment