Mikoa 18
kati ya 27 ya kisoka tayari imeshapata mabingwa wao kwa ajili ya Ligi ya
Mabingwa wa Mikoa itakayoanza Mei 12 mwaka huu chini ya usimamizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF).
Timu tatu za
juu katika Ligi hiyo ya Mabingwa zitapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao
(2013/2014).
Ligi ya FDL
ina jumla ya timu 24 ambapo tatu katika ligi hiyo zilizoshuka daraja msimu huu
wa 2012/2013 ni pamoja na Moro United ya Dar es Salaam, Small Kids ya Rukwa
na Morani FC ya Manyara.
Mabingwa
waliopatikana hadi sasa na mikoa yao kwenye mabano ni Abajalo SC (Dar es Salaam
2), Biharamulo FC (Kagera), Flamingo SC (Arusha), Friends Rangers (Dar es
Salaam 3), Katavi Warriors (Katavi), Kiluvya United (Pwani), Kimondo FC (Mbeya)
na Machava FC (Kilimanjaro).
Wengine ni
Magic Pressure FC (Singida), Mbinga United (Ruvuma), Mji Njombe (Njombe),
Polisi Jamii Bunda FC (Mara), Red Coast FC (Dar es Salaam 1), Rukwa United
(Rukwa), Saigon FC (Kigoma), TECKFOLT FC ya Kilombero ambayo ni Shule ya
Sekondari (Morogoro) na UDC FC ya Ukerewe (Mwanza).
Kila klabu
inatakiwa kulipa ada ya ushiriki ambayo ni sh. 100,000 wakati usajili wa
wachezaji wa timu hizo ni uleule uliofanyika katika Ligi ya Mkoa na unatakiwa
kuwasilishwa TFF kwa ajili ya uthibitisho.
TFF inapenda kusisitiza kuwa hakuna usajili mpya wa
wachezaji kwa ajili ya ligi hiyo.
No comments:
Post a Comment