Askari
wakimuamuru Lwakatare kuondoka kizimbani kwa ajili ya safari ya gerezani.
|
Lwakatare
Akiwaonyesha wafuasi wake wa CHADEMA alama ya ushindi wa chama chao.
|
Ulinzi ndani
ya Mahakama Kuu ya Tanzania Ukiwa umeimarishwa.
|
Ndugu, Jamaa
na Wafuasi wa CHADEMA wakikumbatiana kwa furaha.
|
Mmoja wa
wanachama wa Chadema akiwapigia simu wenzake kuwapasha kilichojiri Mahakamani.
|
Mkurugenzi
wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare akirudishwa rumande kwa kosa moja la kutaka
kumwekea sumu, Dennis Msaki.
|
Mahakama Kuu
ya Tanzania imefuta mashitaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanawakabili Mkurugenzi
wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare na mwenziye Ludovick Joseph.
Taarifa
zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la kula njama ya kuteka na
kudhuru, kosa ambalo kimsingi ni la
jinai na lenye dhamana.
Taarifa
zaidi zinasema kuwa watuhumiwa wamerudishwa rumande kwa kuwa dhamana haikuwa
imeandaliwa.
Akizungumza
na wanahabari Wakili wa mshitakiwa huyo, Peter Kibatara, amesema wanatarajia
kumtoa kwa dhamana mteja wake huyo siku ya Jumatatu ambayo anaamini kuwa
taratibu zote zitakuwa zimekamilishwa.
Katika kesi
hiyo, Lwakatare anawakilishwa na jopo la mawakili watano ambao ni Mabere
Marando, Tundu Lissu, Prof. Abdallah Safari, Peter Kibatala na Nyaronyo
Kicheere.
No comments:
Post a Comment