Watu wawili wamefariki papo hapo baada ya pikipiki na basi la Otraco kugongana eneo la Buhororo wilayani Ngara mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, April 22, 2013

Watu wawili wamefariki papo hapo baada ya pikipiki na basi la Otraco kugongana eneo la Buhororo wilayani Ngara mkoani Kagera.


Ajali hiyo ilihusisha basi la  Otraco la nchini Burundi lenye namba za usajili C 144 AGB lililokuwa likitoka Jijini Mwanza kwenda Jijini Bujumbura nchini Burundi, kugongana uso kwa uso na Pikipiki aina ya SANLG yenye namba za usajili T 403 CAG.




Katika Ajali hiyo iliyotokea (April 21,2013)  cha Buhororo wilayani Ngara mkoani Kagera ,Watu wawili walifariki papo hapo  waliokuwa  kwenye Pikipiki hiyo .





Kwa Mujibu wa Mashuhuda wa Ajali hiyo wamesema  chanzo cha ajali hiyo ni wapanda pikipiki hao walikuwa wakiongea na dereva wa lori  huku wakiwa  kwenye mwendo.




Imeelezwa  waliofariki katika ajali hiyo ni Emily Benjamini na Ayoub Eliphazi na miili ya waliofariki imehifadhiwa katika hospitali ya Nyamiaga wilayani Ngara,mkoani Kagera.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad