PICHA:Jinsi basi la Magu Logistics lilivyopata Ajali leo(April 22,2013) asubuhi katika eneo la Kojifa nje kidogo ya mji wa Ngara mkoani Kagera na kusababisha kifo cha Mtu mmoja na wengine Kujeruhiwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, April 22, 2013

PICHA:Jinsi basi la Magu Logistics lilivyopata Ajali leo(April 22,2013) asubuhi katika eneo la Kojifa nje kidogo ya mji wa Ngara mkoani Kagera na kusababisha kifo cha Mtu mmoja na wengine Kujeruhiwa.



Katika ajali hiyo ya  leo(April 22,2013) asubuhi katika eneo la Kojifa nje kidogo ya mji wa Ngara mkoani Kagera, barabara kuu ya Isaka Bujumbura ni Utingo wa basi hilo  amepoteza maisha na wengine kujeruhiwa kufuatia.




Basi hilo lilikuwa katika safari zake za kawaida  kutoka  wilayani Ngara kuelekea mjini Bukoba mkoani Kagera na chanzo cha ajali hiyo ni kushindwa kufanya kazi kwa mfumo wa breki.



Basi namba T 384 AZJ likiwa limeanguka mita kadhaa kutoka barabara kuu ya Isaka -Bujumbura kupitia wilayani Ngara mkoani Kagera  ambapo chanzo chake ni kushindwa kufanya kazi vizuri kwa mfumo wa breki.







Askari wa Usalama Barabarani akipima umbali wa eneo la ajali kutoka usawa wa barabara ,ajali ambayo imelihusisha basi la Magu Logistics namba T 384 AZJ liliokuwa likifanya safari kutoka Wilayani Ngara kwenda Mjini Bukoba mkoani Kagera leo(April 22,2013) saa Moja asubuhi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad