Watu 73
wenye ulemavu wa ngozi (albino), wameuawa kwa nyakati tofauti katika kipindi
cha miaka sita iliyopita kuanzia mwaka 2007 hapa nchini.
Kwa Mujibu wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali
la Under the Same Sun (UTTS), katika maadhimisho ya miaka
minne tangu kuanzishwa kwake. Under the Same Sun, ilianzishwa nchini mwaka 2008
na kusajiliwa rasmi Aprili 6 mwaka 2009.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti, viongozi wa washirika hilo walisema kuwa mbali na mauaji
hayo, watu wengine 34 wamejeruhiwa kwa kukatwa viungo mbalimbali vya miili yao,
ikiwamo mikono na vidole, huku makaburi 19 yakifukuliwa kutafuta viungo vya
wengine waliouawa na kuzikwa.
“Kinachotusikitisha
ni kwamba pamoja na kasi hiyo ya mauaji, ni kesi nne tu ndizo zilisikilizwa
mahakamani na kutolewa uamuzi. Sisi haturidhiki na kasi ya kusikiliza kesi za
mauaji ya wenzetu wenye albinism,” alisema ofisa uhusiano wa shirika hilo Kondo
Seif.
Kondo
alisema Under the Same Sun imekuwa ikikutana na changamoto nyingi katika
utendaji wake wa kazi ikiwamo jamii kuwanyanyapaa watu wenye ulemavu.






No comments:
Post a Comment