![]() |
| wilayani Ngara |
Afisa
mtendaji wa kijiji cha Rwinyana Bw.Venace
Jonh amemtaja mtu huyo kuwa Jeremo Onesimo mkazi wa kitongoji cha
Nageli kijijini humo.
Amesema
tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo baada ya mtu huyo kukutwa kando ya barabara
akiwa amepoteza maisha huku akiwa na mfuko wa mahindi kilo 20.
Kijana
wa marehemu huyo Nuwaka Pambano amesema
awali baba yake huyo alikwenda kusaga jana jioni kilomita 2 kutoka nyumbani
baada ya hapo alianguka kutokana na pombe alizokuwa amekunywa.
Kufuatia
hali hiyo kijana huyo alimsogeza kando ya barabara ili arudi nyumbani na ndipo
alimwambia akipata nguvu atarudi nyumbani ambapo baadae amekutwa amefariki dunia.
Jeshi
la polisi wiyalani Ngara limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.






No comments:
Post a Comment