Ushindi wa leo wa Yanga SC waivua rasmi Simba SC Ubingwa wa Ligi kuu soka Vodacom Tanzania bara 2012/2013 huku Mechi tano kati ya sita za Super Week hazitaoneshwa kutokana na matatizo ya kiufundi.. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, April 13, 2013

Ushindi wa leo wa Yanga SC waivua rasmi Simba SC Ubingwa wa Ligi kuu soka Vodacom Tanzania bara 2012/2013 huku Mechi tano kati ya sita za Super Week hazitaoneshwa kutokana na matatizo ya kiufundi..



Leo (April 13,2013) ndani ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga waliichapa JKT Oljoro kwa Bao 3-0 na kuzidi kujizatiti kileleni mwa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara, wakiwa Pointi 6 mbele ya Timu ya Pili Azam FC yenye Pointi 46.




Ushindi wa leo pia umeivua rasmi Simba SC Ubingwa kwa vile wana Pointi 35 na wamebakiza Mechi 5 na hata wakishinda zote watafikisha Pointi 50 ambazo Yanga SC wameshazipita.




Mabao yote ya Yanga SC yalifungwa Kipindi cha Kwanza -Dakika ya 5 na Nadir Haroub ‘Cannavaro’,-Dakika ya 19  Simon Msuva na -Dakika ya 43  Hamis Kiiza.



MSIMAMO:


NA
TIMU
p
W
D
L
GD
PTS
1
Yanga SC
22
16
4
2
28
52
2
Azam FC
22
14
4
4
22
46
3
Kagera Sugar
22
10
7
5
7
37
4
Simba SC
21
9
8
4
11
35
5
Mtibwa Sugar
23
8
9
6
2
33
6
Coastal Union
22
8
8
6
3
32
 



Ligi hiyo ya VPL itaendelea kesho (April 14,2013) Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa Mechi ngumu kati ya Simba SC na Azam FC na kipigo kwa Azam FC kitaifagilia Yanga SC kutwaa Ubingwa.




Katika hatua Nyingine  Mechi tano kati ya sita za Super Week za Ligi Kuu ya Vodacom zilizokuwa zioneshwe moja kwa moja (live) na Kituo cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini sasa hazitaoneshwa kutokana na matatizo ya kiufundi.




Kwa mujibu wa Mtayarishaji Mtendaji (Executive Producer) wa SuperSport Kanda ya Afrika, Max Tshunungwa ambaye yuko nchini, wameshindwa kuonesha mechi hizo kutokana na matatizo ya kiufundi katika magari yao ya kurushia matangazo (OB van) yanayohudumia Afrika Mashariki- Kenya, Tanzania na Uganda.




Mechi hizo ni kati ya Azam na African Lyon, Yanga na Oljoro JKT, Azam na Simba, Coastal Union na JKT Ruvu na Mgambo Shooting na Yanga itakayochezwa Aprili 17 mwaka huu jijini Tanga.




Tatizo hilo pia limeathiri mechi za Ligi Kuu ya Kenya (KPL) ambazo hazitaonekana wikiendi hii. SuperSport ndiyo yenye haki za matangazo ya televisheni kwa ligi hiyo ya Kenya.




Tshunungwa amekutana na Sekretarieti ya TFF na Kamati ya Ligi kuelezea tatizo hilo. SuperSport kwa kushirikiana na Kamati ya Ligi na TFF watapanga mechi nyingine za Super Week kabla ya ligi kumalizika msimu huu.




Pia TFF, Kamati ya Ligi na SuperSport watakuwa na mkutano mfupi wa waandishi wa habari wakati wa mapumziko kwenye mechi ya leo kati ya Yanga na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad