![]() |
|
Spika
wa Bunge Anna Makinda
na
Naibu
wake Job Ndugai .
|
Katika
wiki mbili za mwanzo za Mkutano wa 11 wa Bunge la Bajeti, vijembe, matusi,
misimamo na maneno ya kuudhi vilitawala bungeni.
Baadhi
ya kauli zilizotolewa na nyingi kuombewa mwongozo wa Spika ni kama ifuatavyo:-
“Tutaliheshimu
Bunge kama taasisi huru, lakini si lilivyo sasa kama taasisi ya CCM,” Freeman
Mbowe-Chadema, Kiongozi wa Upinzani.
“Sugu siongei na mbwa bali naongea na
mwenye mbwa.” Juma Nkamia-CCM.
![]() |
| Freeman Mbowe |
“Ni
wazi kuwa hata kauli ya Waziri Harrison Mwakyembe imejaa utupu usio na matendo
kwa kukataza wasafiri njiani wasichimbe dawa.” Halima Mdee-Chadema.
“Kuna
wabunge humu ambao wana mimba zisizotarajiwa bungeni.” Livingstone Lusinde-CCM.
“Ukiangalia
kuna watu wanataka kuvuruga nchi wakati wana watoto wachanga. Mimi mtoto wangu
wa mwisho ana miaka minane, halafu Slaa (Dk Willibrod Slaa) wa kwake sijui ana
wiki ngapi.” Livingstone Lusinde.
“Mbowe
kaja hapa kajamba bungeni halafu kakimbilia kwenda kujamba Kibaha.” Mbunge wa
Konde (CUF), Khatibu Said Haji Konde (CUF).
“Sikujua
wabunge mnataka kuvuana nguo, hivyo nitatoa mwongozo wangu baadaye.” Job
Ndugai, Naibu Spika.
Mbunge
wa Iringa Mjini (Chadema), Peter Msigwa alisema, “Kuna tatizo la akili ndogo
kutawala akili kubwa na hilo ni tatizo la Serikali.”
![]() |
| Bungeni Dodoma. |
“Serikali
si sikivu na imevaa miwani ya mbao,” alisema Deo Filikunjombe-CCM.
“Wanapoongea
watoto wa kiume, watoto watulie.” Mwigulu Nchemba-CCM.
“Hatupendi
kusema ufanisi wake umepungua wala kuendelea kubaki ofisini bila ya mkataba ni
kutokana na kujipendekeza kwa Rais na uhodari wake wa kukipendelea chama tawala
na Serikali, lakini tunapenda kusema wapo watu wenye sifa ya kuwa Msajili wa
Vyama vya Siasa.” Profesa Kulikoyela Kahigi.
Chanzo:Mwananchi
na Mwana wa Makonda.








No comments:
Post a Comment