Timu ya Ngara starz hapo jana (April 14,2013) imekubali
kufumuliwa bao 1 -0 katika uwanja
wake wa Nyumbani wa Kokoto,uliopo mjini
Ngara ,kutoka kwa wageni timu ya
Mukombozi FC ya wilayani Muleba
ambayo ilikuja kucheza mchezo huo wa kirafiki pamoja na kudumisha
Ujirani mwema baina ya timu hizo mbili.
Katika mchezo huo
goli hilo moja la wageni Mukombozi FC lilifungwa na mchezaji wao Renatus
Jeremia na kumfanya kocha wa timu hiyo
Dioniz Mutechura kusema kuwa Ngara starz wangewafunga magoli
mengi ila uchovu wa safari kutoka Muleba hadi Ngara ndio uliowafanya kucheza
chini ya kiwango.
Kwa upande wake Kiongozi wa Ngara Starz –Baraka
Abbas amesema wamekubali kipigo hicho na
kusema kuwa bado wako katika mikakati ya kuijenga timu yao .
Aidha Mwenyekiti wa Klabu ya Mukombozi FC Nalisisi Paulo ameishukuru timu ya Ngara starz kwa mapokezi
mazuri waliyowapatia na kuwapa mwaliko
wa kuwatembelea lengo ni kudumisha urafiki wao wa kimichezo kwa Ngara
starz na Mukombozi FC.
|
No comments:
Post a Comment