![]() |
|
Hii
ndio ajali ya ndege iliyochukua
uhai
wa "Babu Sembeke".
|
Mfanyabiashara
mashuhuri mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, Peter Joseph (49), maarufu ‘Babu
Sembeke’, amefariki dunia katika ajali ya ndege.
Sembeke
alikuwa rubani katika ndege hiyo aina ya Cessnar, yenye namba za usajili 5H
–QTT na alikuwa peke yake ndani ya
ndege. Alipata ajali katika eneo la Kisongo, nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Kwa
mujibu wa mashuhuda waliozungumza na mwandishi,
ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiri 4, iliparamia tawi la mti mkubwa
uliopo eneo hilo juzi saa 12.40 jioni.
Mashuhuda
hao walidai Babu Sembeke alipata ajali hiyo, wakati akiwa katika harakati za
kukata kona ili apate mwelekeo mzuri wa kutua katika uwanja wa ndege wa Arusha
uliopo Kisongo jijini Arusha.
Walidai
baada ya kuparamia mti huo na kupoteza mwelekeo, ndege hiyo ambayo ilinunuliwa
kutoka kwa mfanyabiashara mashuhuri wa Arusha, Nyaga Mawalla (38) ambaye
alifariki hivi karibuni jijini Nairobi, ndege hiyo ilianguka papo hapo na
kusababisha majeraha sehemu za kichwani za Sembeke.
"Sembeke
alikufa njiani akipelekwa hospitalini, alikuwa na majeraha makubwa kichwani,’’
alisema mtoa habari.
Sembeke
alikuwa akimiliki ndege mbili pamoja na hiyo iliyopata ajali na nyumba za
kifahari Arusha, Dar es Salaam na Moshi.







No comments:
Post a Comment