Mwigizaji ‘Ray’, asalimu amri filamu yake ya ‘’Sister Mary’’ iliyokuwa imezuiwa kwa kudaiwa kudhalilisha ukatoliki. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, April 05, 2013

Mwigizaji ‘Ray’, asalimu amri filamu yake ya ‘’Sister Mary’’ iliyokuwa imezuiwa kwa kudaiwa kudhalilisha ukatoliki.



Cover la filamu hiyo

ya Sister Marry.
Hatima ya filamu ya mwigizaji, Vincent Kigosi ‘Ray’, Sister Mary iliyokuwa imezuiwa kwa kudaiwa kudhalilisha ukatoliki, imefahamika kuwa mwigizaji huyo amesalimu amri ya viongozi wa kanisa hilo.




Kanisa Katoliki nchini linaloongozwa na Muadhama Polycarp Kadinali Pengo, liliizuia filamu hiyo kwa kile kilichodaiwa kuwa ilikuwa ikionesha udhalilishaji kwa namna ambavyo watawa wamevaa mavazi mafupi. 




Baadhi ya vipande

vilivyomo katika filamu hiyo.
Akipiga stori na paparazi wetu, Ray amebainisha kuwa baada ya kuambiwa achomoe vipande vingi kwenye filamu hiyo, ameona ni bora kuachana nayo kwani hata akitoa haitaleta maana hivyo atakujairudia upya wakati mwingine. 





Asilimia 85 ya filamu niliigizia kanisani na ndivyo walivyosema niviondoe, sina ujanja kwa sasa nimeanza kushuti filamu nyingine kabisa ile labda nije kuirudia upya hapo baadaye,” alisema Ray.




Na Mwandishi Wetu: GPL
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad