Kutokana na
hali hiyo, shirika hilo limesema kwamba asilimia 95 ya watu duniani hawapati
virutubisho vinavyohitajika mwilini na asilimia 75 hula vyakula ambavyo
huwaletea madhara zaidi mwilini kuliko faida.
Kutokana na ukweli huo, maradhi
yataendelea kuongezeka na tutaendelea kuteseka kiafya mpaka hapo tutakapokubali
kubadili staili zetu za ulaji.
BILA shaka
ubongo ni miongoni mwa viungo muhimu vya binadamu lakini ni watu wachache sana
wanaoutilia maanani. Ubongo ndiyo kiungo kinachohusika na utendaji kazi wote wa
mwili na ndiyo unaowezesha mwili kuishi maisha ya furaha au karaha.
Chakula ni
moja ya sababu za msingi kabisa za kuimarisha ufanisi wa ubongo na kuzuia
magonjwa mengine ya akili. Lakini kwa bahati mbaya watu wengi hawajui wale
vyakula gani kwa lengo la kujenga akili na kuimarisha ubongo.
Ifuatayo ni
orodha ya vyakula ambavyo vinaongoza kwa kuimarisha utendaji kazi mzuri wa
ubongo:
MAFUTA YA
SAMAKI
Mafuta ya
samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa fahamu. Ulaji wa samaki wenye minofu
kama samoni (salmon) na dagaa, utaweza kupata faida hizo kwa sababu aina hii ya
samaki ina kiasi kingi cha mafuta ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na
mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili moja kwa moja.
PILIPILI
KALI
Pilipili
kali nayo huwa ni chakula kikubwa cha ubongo kwa sababu ina kiwango kingi cha
Vitamin C ambayo huhitajika zaidi kwenye ubongo, pilipili inaaminika kuwa na
kiwango kingi cha vitamin hiyo kuliko hata machungwa.
MBEGU ZA
MABOGA
Mbegu za
maboga zina kiwango kingi cha madini ya ‘Zinc’ ambayo husadia kuongeza
kumbukumbu (memory). Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga, moja wapo ni
kuzikaanga na kula kama karanga, ukila kiasi cha kiganja kimoja kwa siku,
inakuwa poa.
NYANYA
Nyanya ni
muhimu sana kwa sababu huzuia magonjwa ya ubongo (brain disease) kutokana na
kuwa na kirutubisho aina ya ‘Lycopene’ chenye uwezo wa kuzuia magonjwa
nyemelezi yanayoweza kutokea. Hivyo ulaji wa nyanya utakusaidia kukupa kinga
dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya akili.
BROKOLI
Brokoli ni
mboga ya majani aina fulani kama maua ya maboga, ambayo nayo inafaida sana
kwenye ubongo, ina vitamin K, C na inatoa kinga ya mwili. Vitamin K inahusika
moja kwa moja na utendaji kazi mzuri wa ubongo na husaidia kuzuia magonjwa
yatokanayo na uzee.
KARANGA
Aina zote za
karanga zina vitamin E, ambayo huzuia tatizo la upotevu wa kumbukumbu na pia
zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini.
MAYAI
Mwisho ni
mayai ya kuku, ambayo yana kirutubisho aina ya Choline. Kirutubisho hiki
huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo tu, hivyo kwa kula mayai (ya kienyeji)
utaweza kuongeza kiwango cha kirutubisho hicho mwilini kwa kiwango kikubwa na
hivyo kuimarisha afya ya ubongo.









No comments:
Post a Comment