Manchester City wamejipa matumaini ya angalau kutwaa Kombe moja Msimu huu kwa kuwabwaga nje Mabingwa watetezi wa FA CUP Chelsea . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, April 15, 2013

Manchester City wamejipa matumaini ya angalau kutwaa Kombe moja Msimu huu kwa kuwabwaga nje Mabingwa watetezi wa FA CUP Chelsea .


Manchester City wamejipa matumaini ya angalau kutwaa Kombe moja Msimu huu kwa kuwabwaga nje Mabingwa watetezi wa FA CUP Chelsea kwa kuwapiga Bao 2-1 kwenye Nusu Fainali iliyochezwa Uwanjani Wembley na wao kutinga Fainali ambapo watacheza na Wigan Ahletics.



Mashabiki wa Chelsea na Man City wakwia wanawasili kucheki mechi Wembley.
Man City  ambao wapo nyuma ya Man United kwa Pointi 15 katika Barclays Premier League  wakiwa wamebakiza Mechi 7 na Man United wamebakiza Mechi 6 huku wakihitaji Pointi 7 kati ya hizo kutwaa Ubingwa, tayari   Manchester United wameshinda Bao 2-0 na sasa kuhitaji Pointi 7 tu katika katika Mechi zao 6 zilizobaki ili watwae Ubingwa wao wa 20 bila kujali Timu ya Pili Man City inapata matokeo gani.


Demba Ba baada ya kufunga goli pekee la Chelsea Dakika ya 66 ya mchezo huo wa nusu fainali ya FA CUP April 14,2013.


Kwa Chelsea  chini ya Meneja wa muda Rafael Benitez, nafasi pekee ya wao kutwaa Taji Msimu huu ni EUROPA LIGI ambapo wapo Nusu Fainali na hapo Aprili 25 watacheza na Basel ya Uswisi katika Mechi ya kwanza na kurudiana Wiki moja baadae.


Man City  wanapewa nafasi ya kutwaa Taji hilo  na hii itakuwa ni mara ya pili katika Misimu mitatu chini ya kocha Roberto Mancini kutwaa FA CUP kwani walibeba Kombe hili katika Msimu wa kwanza wa Mancini wa 2010/11.



FA CUP-FAINALI



Jumamosi Mei 11,2013.


Wigan v Man City


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad