Simba SC wairuhusu Azam FC kupata sare ya Bao 2-2 katika Mechi ya Ligi Kuu Vodacom, matokeo ambayo yamewafanya Vinara wa Ligi Yanga SC kuhitaji ushindi kwenye Mechi 2 tu kati ya 4 walizobakiza ili kuwa Bingwa . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, April 15, 2013

Simba SC wairuhusu Azam FC kupata sare ya Bao 2-2 katika Mechi ya Ligi Kuu Vodacom, matokeo ambayo yamewafanya Vinara wa Ligi Yanga SC kuhitaji ushindi kwenye Mechi 2 tu kati ya 4 walizobakiza ili kuwa Bingwa .


Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Simba SC waliumwaga uongozi wa Bao 2-0 na kuiruhusu Azam FC kupata sare ya Bao 2-2 katika Mechi ya VPL, Ligi Kuu Vodacom, matokeo ambayo yamewafanya Vinara wa Ligi, Yanga SC , kuhitaji ushindi kwenye Mechi 2 tu kati ya 4 walizobakiza ili kuwa Bingwa bila kujali matokeo ya Azam FC.


Mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngasa (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Azam Fc, David Mwantika, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya mabao 2-2.

Mwinyi Kazimoto (kulia) akijaribu kuwatoka mabeki wa Azam Fc, wakati wa mchezo huo.


MECHI WALIZOBAKISHA YANGA.



Aprili 17: MGAMBO JKT v YANGA [MKWAKWANI]



Aprili 21: YANGA v JKT RUVU [UWANJA wa TAIFA]



Mei 1: COASTAL v YANGA YANGA [MKWAKWANI]



Mei 18: YANGA v SIMBA [UWANJA wa TAIFA]




MSIMAMO.



NA TIMU p W D L GD PTS
YANGA  22  16  4 2 28 52
2 Azam FC 23 14 5 4 22 47
3 Kagera Sugar 22 10 7 5 7 37
4 Simba 22 9 9 4 11 36
5 Mtibwa Sugar 23 8 9 6 2 33
6 Coastal Union 22 8 8 6 3 32
7 Ruvu Shooting 22 8 6 8 0 30
8 JKT Oljoro 23 7 7 9 -4 28
9 Prisons FC 24 6 8 10 -7 26
10 Mgambo Shooting 22 7 3 12 -7 24
11 Toto African 24 4 10 10 -11 22
12 JKT Ruvu 21 6 4 11 -15 22
13 Police M 23 3 10 10 -10 19
14 African Lyon 23 5 4 14 -19 19



**TEBO toka TFF [Tanzania Football Federation]


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad