Leo ni kumbukumbu ya Mwaka mmoja toka Mwigizaji Steven Kanumba afariki tarehe 07.04.2012. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 07, 2013

Leo ni kumbukumbu ya Mwaka mmoja toka Mwigizaji Steven Kanumba afariki tarehe 07.04.2012.


Waigizaji mbalimbali kwenye kumbukumbu ya Marehemu Kanumba makaburini Kinondoni  ikiwa ni siku  ambayo Familia yake wameiita Kanumba day ambapo wamekutana kanisani kwa misa kanisa la kilutheri huko kimara pamoja na kula chakula cha mchana.







Aidha Jioni pale leades itaonyeshwa filamu yake ya mwisho aliyoigiza kabla hajafariki.



Wapezi,wadau wote mnaweza kujitokeza kwani ni bure.


The Great Steven Kanumba atakumbukwa kama mmoja ya wasanii waliofanya tasnia ya filamu nchini izidi kukua na kupendwa hadi kuteka soko ambalo kwa kiasi kikubwa lilikuwa likishikiliwa na wasanii wa Nigeria.


Aliondoka wakati bado hajayafaidi mafanikio na kushuhudia namna mapinduzi aliyofanya yalivyotengeneza ajira kwa vijana wengi.


Pumzika kwa amani The Great Steven Kanumba.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad