![]() |
| Jose Mourinho |
Kocha Jose
Mourinho ameitaka Chelsea kuthibitisha kurejea kwake Stamford Bridge au
kujiweka hatarini kumkosa.
Kocha huyo
wa Real Madrid anatarajiwa kumpokea majukumu Rafa Benitez mwishoni mwa msimu
hiyo ikiwa mara ya pili kwake kufanya kazi Ligi Kuu England.
Lakini
Manchester City, Paris Saint-Germain na AC Milan pia zimeripotiwa kumsubiri
mkali huyo wa mataji.
Muda
unakimbia: Jose Mourinho amejiandaa kurejea Chelsea mwishoni mwa msimu.
"Jose
anataka kurudi Chelsea. Ni mahali anapotaka kuwa," chanzo kimeiambia The
Sun.
"Kila
wakati mashabiki wa Chelsea wanaimba jina lake na hiyo inamfanya atake kurejea
hata zaidi.
"Atasaini
kwa dau lile analopata Real, pamoja na kwamba ana uhakika wa kupata zaidi
sehemu nyingine — kama City au PSG.
Real Madrid wakianza
bila Nyota wao Ronaldo, Real walijikuta wakitanguliwa Bao 1-0 na Levante katika
Mechi iliyochezwa Uwanjani Santiago Bernabeu lakini walizinduka na kufunga Bao
mbili za haraka kupitia Gonzalo Higuain na Penati ya Kaka.
Ronaldo
aliingizwa Kipindi cha Pili na kupiga Bao moja na nyingine mbili kuongezwa na
Mezut Ozil.
Jumanne
ijayo Real Madrid watakuwa huko Uturuki kurudiana na Galatasaray katika
Robo Fainali ya UEFA huku wao wakiwa washindi wa Bao 3-0 katika Mechi ya
kwanza.
"Jose
anaweza pia kubaki Madrid, lakini yuko wazi juu ya wapi anapotaka kwenda — sasa
ipo juu ya Roman Abramovich ikiwa anataka hivyo.'
Mourinho
ameshinda mataji sita na Chelsea ndani ya misimu mitatu, lakini hakuweza kutwaa
taji la Ligi ya Mabingwa.
Anatarajia
kufanya hivyo Uwanja wa Wembley, Mei 25 akiwa na Real Madrid ambayo ina
matumaini ya kuingia Nusu Fainali baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Galatasaray
wiki iliyopita.
Safari
inanukia: Rafa Benitez anatarajiwa kuachia ngazi mwishoni mwa msimu.
Benitez
hajawahi kukubalika kwa imani za Chelsea, baada ya kuchukua mikoba ya Roberto
Di Matteo, aliyetupiwa virago.
Mspanyola
huyo ameweka bayana ataachia ngazi mwishoni mwa msimu, lakini atakuwa bado
hajatwaa mataji ya Europa League na Kombe la FA.








No comments:
Post a Comment