![]() |
|
aina
mbalimbali ya mahindi
|
Waziri wa
Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, amebainisha hayo alipokuwa
akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka
wa fedha 2013/14 bungeni mjini Dodoma.
Chiza
alisema kuwa pamoja na halmashauri hizo kukabiliwa na njaa, 47 kati ya hizo
ziko katika hali ya ukame zaidi na kuifanya serikali kuhakikisha inatenga tani
69,452 za chakula ili kuwanusuru wananchi.
Alisema
tathmini iliyofanywa na serikali kwa kipindi cha Septemba 2012 na Januari 2013,
ilibaini kuwa halmashauri 47 katika mikoa 19 zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa
chakula kutokana na hali ya ukame.
Chiza
aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Arusha, Kilimamnjaro, Manyara, Morogoro, Lindi,
Tanga, Mtwara, Pwani , Shinyanga, Simiyu, Tabora, Mwanza, Mara, Kagera, Iringa,
Mbeya, Rukwa, Dodoma na Singida.
Alieleza
kuwa njaa katika halmashauri hizo inatokana na ukosefu wa mvua za vuli katika
robo ya nne ya mwaka 2011/12 pamoja na upungufu wa chakula katika nchi jarani
na zile za Sudan Kusini na hivyo kusababisha mfumko wa bei za vyakula.
Waziri
aliongeza kuwa kutokana na kuwepo kwa hali ya njaa katika maeneo mbalimbali
nchini, serikali imeidhinisha chakula cha msaada tani 69,452.
Pia alikiri kuwa
kuwepo kwa miundombinu mibovu kumewasababishia wakulima kushindwa kuuza mazao
yao katika masoko mazuri na badala yake wamekuwa wakiuza kwa wafanyabiashara
wasio waaminifu.
Alisema kuwa
pamoja na serikali kuweka utaratibu wa kuimarisha kilimo, bado vijana wengi
wanakimbilia mijini badala ya kujihusisha na sekta hiyo.
Katika
bajeti yake, wizara imeomba kiasi cha sh 328,134,608,000 kwa ajili ya matumizi
ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2013/14.
Mchanganuo
wake ni kwamba sh bilioni 247 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh bilioni
81 ni kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Chiza
alisema katika matumizi ya kawaida sh bilioni 210.1 ni kwa ajili ya matumizi
mengine, sh bilioni 25.6 (mishahara ya wizara) na sh 11.3 (mishahara ya bodi na
taasisi).
Alisema kuwa
kati ya fedha za bajeti ya maendeleo sh bilioni 23.9 ni fedha za ndani na sh
bilioni 57.1 ni za nje.
Nayo Kamati
ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, imeishauri serikali kuongeza bajeti ya
wizara hiyo kwa madai kuwa iliyotengwa kwa mwaka ujao ni ndogo na haiwezi
kuleta tija.
Katika maoni
yao, kamati ilisema kuwa ukuaji wa kilimo nchini unashuka mwaka hadi mwaka kama
inavyoonyeshwa katika takwimu mbalimbali tangu mwaka 2009 hadi ifikapo 2014.
Kutokana na
mtiririko wa kushuka kwa ukuaji wa kilimo, kamati iliishauri serikali
kuhakikisha inafanya uamuzi wa makusudi ili bajeti ya sekta ya kilimo ifikie
kiwango kilichokubaliwa na nchi za SADC cha asilimia 10 ya bajeti ya serikali
ili kilimo kiweze kuchangia kikamilifu katika uchumi wa taifa.
Akisoma
maoni hayo, Prof. Peter Msollwa, alisema kamati ilipendekeza serikali kuongeza
ruzuku ya pembejeo kwa wakulima ya sh 66,326,180,000 kama utaratibu wa vocha
utatumika kutoa ruzuku na sh 108.508,500,000 kama utaratibu wa mikopo utatumika
kutoa ruzuku.
Pia
waliitaka serikali kulipa madeni ya wizara yanayofikia sh 20,326,323,310 ambayo
yanahusisha wazabuni mbalimbali katika kipindi cha mwaka 2010/2011 na 2011/12.






No comments:
Post a Comment