Wakati idadi
ya wanawake wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ikiongezeka, asilimia 26.5 ya
wanawake Tanzania wamebainika kuwa wanafanya mapenzi kinyume na maumbile.
Mfumo wa Uzazi
Unaharibika.
Watafiti
wanabainisha kuwa kitendo hicho licha ya ukweli hakifai kwa vile kinaharibu
mfumo wa uzazi, kina athari kubwa mno kwa mwanadamu, moja wapo ikiwemo
uwezekano mkubwa wa wahusika kuambukizana virusi vya Ukimwi kwa vile hakuna
vilainishi, hivyo kusababisha michubuko ambayo ndio njia kuu ya kuambukiza vijidudu
hivyo.
Mtafiti Mwanasayansi, Irene Mremi kutoka Taasisi ya
Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu nchini Tanzania (NIMR) alitoa ripoti
hiyo hivi karibuni hapa jijini Dar Es Salaam.
Mremi akiwa
na jopo la watafiti kutoka NIMR anasema kuwa wanawake hao wamesema chanzo
kikubwa kinacho wapelekea kufanya ngono kinyume na maumbile ni kujipatia kipato
zaidi na Kuogopa kupata Mimba.
Vilevile alizitaja sababu nyingine za wanawake
kufanya mapenzi kwa njia hiyo ni kulinda usichana wao na baadhi ya mila na tamaduni
za baadhi ya makabila.
Sampuli za Utafiti.
Utafiti huo
ulikusanya sampuli kutoka katika mikoa ya Dar es salaam, hasa maeneo ya
Kinondoni, Tanga, Makete na Siha.
Mremi anasema “Utafiti wetu uliwahusisha
wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea na kada tofauti
katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wahudumu wa bar, wauguzi, makahaba na
akina mama wa nyumbani.
Katika
maeneo hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo pia wanaume ambao walihusishwa
katika utafiti huo.
Imani potofu
kwa Wanaume.
Wanaume
waliohojiwa wamesema wanafanya kwa ajili ya kupata raha tu na imani ya kuwa
huko hakuna maaambukizi ya VVU, kitu ambacho ni uongo, kwani huko ndiko kwenye
kuchangia ukimwi kwa haraka zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote.
Source:Mwananchi.







No comments:
Post a Comment