![]() |
| Bw.Mizengo
Pinda Waziri Mkuu wa Tanzania |
Waziri Mkuu wa Tanzania Bw.Mizengo
Pinda amewataka Watanzania kuzingatia matumizi ya uzazi wa mpango ili
kukabiliana na ongezeko la watu ambalo linatarajiwa kufikia milioni 90 mwaka
2050.
Akizindua ripoti ya idadi ya
watu katika ngazi ya taifa, wilaya, kata na shehia, wiki hii jijini Dar es Salaam,
Waziri Pinda alisema ni vyema kuzingatia uzazi wa mpango kama
ilivyoainishwa katika sera ya watu ya mwaka 2006.
Alisema ni vyema Watanzania
wakaachana na dhana potofu kuwa kuzaa watoto wengi ni umaarufu na utajiri.
Desemba 31, mwaka jana, Rais
Jakaya Kikwete alizindua matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi kwa mwaka 2012
ambapo idadi ya Watanzania ilifikia milioni 44.9.
Matokeo hayo yalionyesha kuwa
wanawake ni asilimia 51 wakati wanaume ni asilimia 49.
Kimkoa, ripoti hiyo
ilionyesha mikoa yenye idadi kubwa ya watu kuwa ni Dar es Salaam wenye idadi ya watu Milioni 4,364,541.
Mwanza 2, 727, 509 na Mbeya 2,707,410.
Pinda alisema, Serikali
itaendelea kushirikiana na wananchi kuhimiza matumizi ya uzazi wa mpango
kutokana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na ongezeko la idadi ya watu.
Vilevile Pinda alisema iwapo
ongezeko la watu la asilimia 2.7 kwa mwaka litaendelea basi idadi ya watu Tanzania
itafikia milioni 90 ifikapo mwaka 2050.
Ripoti hiyo ilionyesha kuwa
Mkoa wa Dar es Salaam
una ongezeko kubwa la watu kwa asilimia 5.6 kwa mwaka ukifuatiwa na Mkoa wa
Mjini Magharibi na Unguja ambapo kasi katika miji hiyo ni asilimia 4.2.
Alisema msongamano wa watu
katika miji hiyo ni mkubwa na unasababisha shinikizo katika utoaji wa huduma za
maendeleo kama maji, elimu, afya, umeme na
miundombinu.






No comments:
Post a Comment