Alirejea ,
mjini Caracas mnamo Februari 18 kwa mara ya kwanza tangu maradhi yake yamzidie
ambapo alipelekwa hospitali ya kijeshi kuendelea kupokea matibau.
Hata hivyo
maelezo zaidi hayakutolewa juu ya afya yake. Waandamanaji waliandamana katika
mji mkuu Caracas mwishoni mwa juma wakidai kuwa watu wa Venezuela wanapaswa
kupewa habari zaidi kuhusu afya ya rais wao.
Afya
Bwana Chavez
amekua uongozini nchini Venezuela kwa miaka 14 na anatazamiwa kuleta mageuzi
makubwa yaliyolenga zaidi kuimarisha maisha ya raia wa pato la chini.
Ujumbe wa
Jeshi
Taarifa
kutoka kwa jeshi imesema kuwa wataendelea kuilinda hadhi ya nchi na kuimarisha
usalama. Pia jeshi limeahidi kuendelea kuwa waaminifu kwa makamu wa rais
Nicholas Marduro na wakatoa wito kwa raia kuwa watulivu.
Chavez - Wasifu
Hugo Chavez
alijitosa katika siasa za Venezuela mnamo Februari 1992 akiwa luteni katika
jeshi.
Aliongoza mapinduzi dhidi ya rais wa wakati huo Carlos Andres Perez.
Lakini
kutokana na kukosa usaidizi wa kutosha wa kijeshi, Chavez na wanamgambo wenzake
walishindwa kunyakua madaraka hayo. Alikiri kushindwa na aliwekwa korokoroni.
Aliingia
uongozini baada ya ushindi mkubwa ulioviondosha vyama vya kisiasa wakati huo.
Katika kuapishwa kwake mnamo February 1999, Hugo Chavez alitangaza wazi kwamba
mipango yake ya mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi sio kampeni tu.
Alitimiza
ahadi yake na kuiongoza nchi hiyo katika mabadiliko ambayo hayakuwahi
kushuhudiwa katika muda wa miongo kadhaa.
Alibadili muundo wa bunge na
kulifanya kuwa la kikatiba, ambalo liliiunda katiba mpya baada ya kura ya maoni
iliyoidhinishwa na 88% ya wapiga kura.
Rais Chavez
alitaifisha rasilmali ukiwemo utajiri wake mkubwa wa mafuta. Sera kama hizi
zilimfanya azozane na kampuni za kimataifa za mafuta, lakini alipata uungwaji
mkono mkubwa wa watu maskini.
Chavez na Jamii ya kimtaifa
Kutokana na
urafiki wake na viongozi wa mrengo wa kushoto kama vile rais wa Cuba, Fidel
Castro, ambaye walikuwa na uhusiano wa karibu aligongana kidiplomasia na
Marekani, ambayo ni mshirika wake mkuu wa kibiashara.
Chavez
alipendwa nyumbani na wafuasi wake lakini alipingwa na baadhi ya watu nchini
humo na katika nchi za nje.
Alionekana sio tu kama bingwa wa jamii maskini
lakini pia kama muingiliaji wa siasa za nchi jirani. Katika miaka ya hivi
karibuni alilenga kukabiliana na masuala ya ndani ya Venezuela, kama uhalifu,
kuinua uchumi wa nchi na kukabiliana na rushwa.
No comments:
Post a Comment