Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya New Habari wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Dimba, Bingwa na
Dimba, Absalom Kibanda amevamiwa na watu wasiojulikana akiwa ndani ya gari lake
wakati akiingia nyumbani kwake Mbezi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Kibanda
alivamia majira ya saa sita usiku wa kumkia leo, akitokea kwenye majukumu yake
ya kila siku. Inadaiwa kuwa alichomolewa kwene gari, akapigwa na vitu vyenye
ncha kali kichwani, ametobolewa jicho lake la kushoto pamoja na kunyofolewa
kucha na baadhi ya vidole na hatimaye kutupwa umbali kidogo ya nyumbani kwake.
![]() |
Absalom Kibanda |
Baada ya
hapo wasamalia wema walijitokeza na kumkimbiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,
ambako alipokelewa vizuri na madaktari na kumpatia tiba ya awali na baadaye
kumhamishia Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) ambako mpaka sasa anaendelea na
matibabu.
Watu
waliomfanyia madhara hayo, hawakuweza kuchukua kitu chochote kwenye gari ambapo
kulikuwemo Laptop, simu na nyaraka zingine.
Blog ya
Mwana wa Makonda inatoa Pole sana
kwa familia ya Kibanda, Mungu atakujalia upate matibabu na kupona haraka. Amin.
No comments:
Post a Comment