![]() |
Azam FC |
Kama
ilivyotarajiwa na wengi, Azam FC ndio timu pekee iliyobaki kwenye michuano ya
Afrika baada ya jioni ya leo(March 03,2013)
kuifunga Al Nasir ya Juba, mabao 5 - 0 kwenye Uwanja wa Juba, Sudan Kusini.
Kwa matokeo hayo, Azam FC inaingia Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa ushindi wa jumla wa mabao 8 - 1, kufuatia ushindi 3 - 1 katika mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita Dar es Salaam.
Aidha
Kuna uwezekano mkubwa Azam FC ikarejea Sudan, kwani katika mchezo wa kwanza, Al
Nasir ililazimishwa sare ya bila kufungana na El Khartoum El Watan.
Katika mchezo huo, mabao ya Azam FC yalifungwa na Kipre Herman Tchetche, John Raphael Bocco kila mmoja mawili, moja kila kipindi na lingine Khamis Mcha ‘Vialli’.
Mapema jioni ya leo(March 03,2013, Jamhuri ya Pemba, imekuwa timu ya kwanza ya Tanzania kuaga michuano ya Afrika, baada ya kufungwa mabao 5-0 na wenyeji Kedus Giorgis nchini Ethiopia katika mchezo wa marudiano, Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika.
Matokeo hayao, yanamaanisha, Jamhuri imeaga kwa kufungwa jumla ya mabao 8-0, baada ya awali kutandikwa 3-0 katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Gombani, Pemba.
![]() |
Simba SC |
Wawakilishi wengine wa Bara katika michuano hiyo na Mabingwa watetezi wa Ligi
kuu soka Vodacom Tanzania Bara , Simba SC wametolewa baada ya kufungwa mabao
4-0 na Recreativo de Libolo ya Angola kwenye Uwanja wa Manispaa mjini Calulo,
Angola.
Matokeo hayo yanaifanya Simba SC itolewe kwa jumla ya mabao 5-0, baada ya awali kufungwa bao 1-0 Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment