|
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kuwa kimeamua kuanza kutekeleza sera yake ya kuongoza kwa majimbo sasa ili kuongeza nguvu ya mapambano na harakati za kuhakikisha wanafanikisha malengo yao ya kushika dola mwaka 2015, badala ya kuendelea kutumia mfumo wa zamani ambao ilikuwa rahisi kudhibitiwa na serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) .
Kadhalika, chama hicho kimesema hakitampokea mwanachama
yeyote wa Chama Cha Mapinduzi atakayekosa nafasi ya kugombea kwenye chama chake
na kutimkia Chadema katika dakika za mwisho kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa
Mwaka 2015.
Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe aliyasema hayo
wakati akizungumza na viongozi wa Chadema wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini
ikiwa ni maandalizi ya kuzindua kanda yake kwenye kanda hiyo.
Alisema kuwa mfumo wa zamani ambao mambo yote ya harakati za
chama hicho yalianzia makao makuu ya chama, ulikuwa ni rahisi kudhibitiwa
na dola ya CCM kwa kuwa walikuwa wakiwavizia viongozi wa kitaifa wanapotoka nje
kwenda kuendesha harakati wanawapiga mabomu, kuwakamata na kuwafungulia kesi
mahakamani.
“Tunataka dola ikusubiri viongozi wa kitaifa watoke makao
makuu ili wawadhibiti, wasikie mapambano yanatokea kwenye kanda zetu kama hii
ya Nyanda za Juu Kusini, kanda ya Magharibi na nyinginezo,” alisema Mbowe.
Alisema kuwa katika mabadiliko hayo pia Chadema inaachana na
siasa za kiuanaharakati na badala yake inaanza kujikita kwenye siasa za
maandalizi ya kushika dola.
Akizungumzia utaratibu wa baadhi ya wanachama wa vyama
vingine, kikiwemo chama tawala CCM kukimbilia ndani ya chama hicho baada ya
kutoswa kwenye nafasi za uchaguzi, Mbowe amesema kuwa kuanzia sasa Chadema
hakitampokea mwanachama yeyote wa aina hiyo.
Sehemu
ya maelfu ya
wananchama wa chadema
mkoani
mbeya wakimsikiliza
mwenyekiti
wa chadema na
mbunge
wa Hai
Freeman Mbowe |
Mbowe alisema kuwa Chadema hivi sasa ipo kwenye maandalizi
makubwa ya kunyakua dola mwaka 2015 na hivyo inao wajibu wa kuwaandaa wanachama
wake ipasavyo ili kiweze kuwa na wagombea wazuri, imara na wenye uwezo wa
kuwezesha chama hicho kupata ushindi mkubwa.
“Kama kuna mtu leo anakula matunda ya ufisadi ndani ya Chama
Cha Mapinduzi akidhani kuwa atahamia Chadema kwa kuwa ana fedha za kununua kura
za maoni, ameula wa chuya, hatutampokea mtu wa aina hiyo, ” alisema Mbowe.
Alisema kuwa kuanzia sasa Chadema itawapokea wanachama kutoka
vyama vingine baada ya kuwapima uadilifu wao, kuchunguza historia yao na
utayari wao wa kutumika ndani ya chama ili waweze kupata wanachama na viongozi
wazuri watakaokisaidia chama kushika dola mwaka 2015.
Alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi kimekuwa kikitumia mbinu
mbalimbali za kukisambaratisha Chadema, ikiwa ni pamoja na kuwatumia mamluki
ndani ya chama, lakini kutokana na uimara wa Chadema mbinu hizo zimekwama na
Chadema inasonga mbele.
Sehemu
ya maelfu ya
wananchama wa chadema
mkoani
mbeya.
|
Alisema kuwa ikiwa wana-Chadema wataruhusu Chadema ife leo,
itawachukua tena miaka 20 mingine kuijenga na kuifikisha mahali iilipo hivi
leo.
Mbowe alitolea mfano wa vyama vya siasa vilivyowahi kupata
nguvu na umaarufu mkubwa wa kisiasa nchini kama vile Chama cha Wananchi, CUF,
NCCR – Mageuzi na TLP ambavyo alidai kuwa CCM illifanikiwa kuvizima na kuwa
hata vyenyewe itavichukua muda mrefu usiopungua miaka 20 kurejesha
umaarufuvilivyokuwa nao.
Mbunge
wa iringa mjini Chadema Mchungaji Peter Msigwa akiunguruma kwneye mkutano wa
chadema Mbeya.
|
Mbunge
wa Mbeya mjini Chadema Joseph Mbilinyi aka Mr II Sugu akiwasha moto kwenye
mkutano wa Chadema Mkoani Mbeya.
|
Sehemu
ya Michango mbalimbali kutoka kwa wanachama na wapenzi wa chadema waliochangia
kampeni ya vuguvugu la mabadiliko (M4C)kwenye mkutano huo wa hadhara.
|
Katika
Hatua Nyingine Kanda ya Ziwa Magharibi
imetangaza kikosi kazi kilichosheni wataalamu wa fani mbalimbali ili kuanza
Utekelezaji kwa Vitendo mkakati wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kugatua madaraka kwa kutafsiri sera yake
ya majimbo, umeanza kazi rasmi katika kanda zake 10.
Freeman Mbowe. |
Kanda
hiyo inayohusisha mikoa ya Geita, Kagera na Mwanza, ilizinduliwa wiki iliyopita
mkoani Mwanza, mbele ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe.
Mkutano
wa uzinduzi wa kanda hiyo uliohudhuriwa na wajumbe wa mabaraza ya uongozi,
wabunge na madiwani kutoka mikoa hiyo, uliwachagua watu sita kuunda timu ya
muda ya uratibu wa kanda kwa miezi mitatu.
Waliochaguliwa
kuongoza kanda hiyo ni Peter Mekere (Mwenyekiti), Dk. Rodrick Kabangila (Makamu
Mwenyekiti), Renatus Bujiku (Katibu), Cecilia Odemba (Mhazini) na Tungaraza
Njugu.
Mekere
ni mtaalamu mshauri wa biashara na utawala na mafunzo ya biashara. Ana shahada ya
biashara na uongozi na stashahada ya ualimu. Ni mwenyekiti wa kamati ya fedha
na mipango ya Shirika la nyumba la Taifa (NHC), Kanda ya Ziwa.
Kabangila
ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Afya, Bugando, daktari bingwa wa
magonjwa ya binadamu na Makamu wa Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).
Ana
shahada ya uzamili ya magonjwa ya wanadamu, shahada ya udaktari, shahada ya
uzamili, epidemilojia na utafiti wa huduma za afya.
Bujiku
ni mwalimu, mtaalamu mshauri, ofisa wa kanda ya ziwa wa shirika la ACORD kwa
muda sasa.
Ana shahada ya uzamili, uongozi na mipango,
shahada ya Elimu, Stashahada ya Maendeleo na misaada ya kiutu.
Njugu
amekuwa Meneja wa shirika la kijamii (CACT-Mwanza 2008-2010), meneja wa Chama
cha Akiba na Mikopo (MWAUWASA SACCOS 2007 hadi sasa) ana cheti cha uhasibu
kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) na cheti cha sheria kutoka
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Odemba
ni Meneja masoko katika usafiri wa anga, mkurugenzi wa kampuni ya uwakala ya
usafiri wa anga, na amewahi kuwa katibu wa kamati ya uhamasishaji ya vuguvugu
la mabadiliko (M4C) kanda ya Ziwa.
Mekere
alisema: “Timu yetu imetokana na watu wenye taaluma mbalimbali ambao wamekuwa
wakitafuta nafasi kukisaidia chama kupitia taaluma zao.
Tunaipongeza
CHADEMA kwa kuanzisha sera ya majimbo kuandaa Watanzania kupata maendeleo kwa
haraka kwani utaratibu huu wa majimbo ya chama unarudisha mamlaka kwa wananchi,
na ni maandalizi ya kuongoza nchi.
“Kwa
utaratibu huu wananchi wamerudishiwa madaraka yao, wana nafasi ya kuamua kuhusu
rasilimali zao na kupanga namna ya kuzitumia. Utaratibu huu unaharakisha
maendeleo tofauti na mfumo wa kimikoa uliowekwa na CCM.”
No comments:
Post a Comment