Utafiti
uliofanywa na Chuo Kikuu cha State cha
jijini New York nchini Marekani unaeleza kuwa manii ni nzuri kwa wanawake kwani
huwaondolea msongo wa mawazo.
Pia,
watafiti hao wamesema wanawake wanaofanya tendo la ndoa mara kwa mara bila
kutumia kinga (mapenzi salama) wanakuwa na kiwango kidogo cha msongo wa mawazo
na hufanya vizuri katika vipimo vya akili.
Hali
hii wamesema wataalam hao kuwa inatokana na manii kuwa na kemikali ambazo
humfanya mtu kuwa vizuri kihisia, huongeza upendo/unyenyekevu, huchochea mtu
kupata usingizi na huwa na angalau aina tatu za kemikali za kuondoa msongo wa
mawazo (anti-depressants).
Utafiti
huo uliofanywa kwa kuwahoji wanawake 293 kwa kufuatilia maisha yao ya kujamiana
dhidi ya afya za akili zao. Manii huwa na mchanganyiko wa kemikali aina ya
cortisol ambayo huongeza upendo, kemikali aina ya esterone na oxytocin ambazo
zote humfanya mtu kuwa vizuri kihisia.
![]() |
msongo wa mawazo |
Pia,
huwa na homoni aina za ‘thyrotropin releasing hormone’, ambayo huondoa msongo
wa mawazo, melatonin ambayo huchochea usingizi na serotonin ambayo ni homoni
inayoondoa msongo wa mawazo.
Kutokana
kuwapo kwa mchanganyiko wa kemikali na homoni hizo kwenye manii.
Matokeo
ya utafiti
Matokeo
muhimu ya utafiti huu ambao umechapishwa katika jarida la ‘Archives of Sexual
Behaviour’ ni kwamba hata baada ya baadhi ya watafitiwa kuongeza kiwango chao
cha kujamiana, wale ambao walikuwa hawatumii kinga yoyote walikuwa na kiwango
kidogo cha msongo wa mawazo tofauti na wale ambao walikuwa wakitumia kinga kama
kondomu wakati wa kujamiana.
No comments:
Post a Comment