![]() |
Yanga
SC
v/s
Kagera
Sugar.
|
Kwa
mara ya pili mfululizo, kiungo Haruna
Hakizimana Fadhil Niyonzima leo(Feb 27,2013) tena amekuwa shujaa wa timu yake ya Yanga SC baada ya kuifungia bao pekee la
ushindi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Niyonzima alijikuta akituzwa fedha na mashabiki wa timu yake baada ya mechi hiyo, iliyokuwa ngumu kwa Wana Jangwani, kutokana na kuibeba timu hiyo mara mbili mfululizo kwa kufunga mabao ya juhudi binafsi, ikiwemo mechi iliyopita dhidi ya Azam FC.
Ushindi
huo unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 42, baada ya kucheza mechi 18, hivyo
kujitanua kileleni mwa Ligi Kuu, ikiizidi Azam FC kwa pointi sita, ambayo
inashika nafasi ya pili kwa pointi zake 36, wakati mabingwa watetezi, Simba SC
wanashika nafasi ya tatu wakiachwa Pointi 11 kwani wana Pointi zao 31.
Kagera Sugar inabaki na pointi zake 28 katika nafasi ya tano, baada ya kucheza mechi 19, chini ya Coastal Union ya Tanga inayoshika nafasi ya nne kwa pointi zake 30.
Hata hivyo, mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Didier Kavumbangu aliikosesha timu yake bao, baada ya kupiga juu ya lango mkwaju wake wa penalti dakika ya 44.
Refa Mberwa, alitoa penalti hiyo baada ya Kavumbangu mwenyewe kudakwa miguu kwenye eneo la hatari na kipa wa Kagera, Mganda Hannington Kalyesebula.
Aidha
Kwa ushindi huo, Yanga imelipa kisasi cha kufungwa 1-0 na Kagera katika mchezo
wa kwanza wa ligi hiyo, mwishoni mwa mwaka jana mjini Bukoba.
Matokeo
Mengine ya Ligi Kuu soka Vodacom Tanzania Bara:-
Castal
Union 0 – 0 Ruvu Shooting.
Mtibwa
Sugara 0 – 0 Tanzania Prisons.
REKODI YA
WACHEZAJI WAPYA YANGA SC:
MCHEZAJI MABAO MECHI
Said Bahanuzi Yanga 13 20 3penalti
D. Kavumbangu Yanga 10 22 1penalti
Simon Msuva Yanga 5 22
Nizar Khalfan Yanga 4 13
Mbuyu Twite Yanga 3 18
No comments:
Post a Comment