Wakiwa
Nyumbani NOU CAMP, FC Barcelona
walichapwa Bao 3-1 na Mahasimu wao wakubwa Real Madrid na kutupwa nje ya COPA
del REY na leo Nyota wao Lionel Messi alishindwa kufanya Mazoezi na wenzake na
Madaktari wa Klabu yake kulazimika kwenda Nyumbani kwake na kumgundua ni
mgonjwa na ana Homa.
Taarifa
iliyotoka kwenye Tovuti ya Barcelona imetamka kuwa Staa huyo alitibiwa na
Madaktari wao na kumshauri apumzike.
Jana
Messi alicheza Dakika zote 90 za kipigo chao toka kwa Madrid na Barcelona na wanaamini atakuwa fiti kucheza
Mechi ya La Liga hapo Jumamosi Uwanjani Santiago Bernabeu dhidi ya Real Madrid.
Barcelona
imethibitisha Alhamisi ni Siku ya Mapumziko kwa Wachezaji na Ijumaa watarudi
Mazoezini ambako Messi anategemewa kuhudhuria.
Msimu
huu, Messi ameichezea Barcelona katika
kila Mechi ya La Liga na kuiwezesha kuwa kileleni wakiwa Pointi 16 mbele ya
Real Madrid ambao ni Mabingwa watetezi.
Wakati
huo huo, Beki wa Barcelona, Jordi Alba, ambae jana ndie alifunga Bao pekee la
Barca walipochapwa 3-1 na Real Madrid - ameeleza kuwa ana imani kwamba kutolewa
kwao nje ya COPA del REY kutawaimarisha katika Mechi ya Marudiano ya Raundi ya
Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, ambapo watacheza Uwanjani Nou
Camp na AC Milan ambao wanatinga hapo wakiwa Washindi katika Mechi ya kwanza
kwa Bao 2-0.
Wiki
iliyopita, katika Mechi ya kwanza iliyochezwa San Siro, Bao za Kipindi cha Pili
za Kevin-Prince Boateng na Sulley Muntari, ziliwapa AC Milan ushindi wa Bao 2-0
dhidi ya Barca na Timu hizi zitarudiana Nchini Spain hapo Machi 12.
Alba
ametamka: “Jana tulicheza kwa nguvu zote lakini haikuwa na kipigo hiki kitatupa
nguvu kuivaa AC Milan. Tumefungwa Mechi mbili muhimu na ni muhimu tupate Goli
la mapema.”
No comments:
Post a Comment