Dk Willibrod Slaa |
Utafiti huo
umeonyesha kuwa endapo uchaguzi huo ungefanyika sasa, Katibu Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa angeibuka mshindi baada ya
kuongoza orodha hiyo akipata asilimia 17.
![]() |
Mizengo Pinda |
Hata hivyo,
licha ya kuongoza, Dk Slaa ameporomoka kwa asilimia 25 ikilinganishwa na
matokeo ya utafiti kama huo uliofanywa na taasisi hiyo mwaka 2011 ambapo
alipata asilimia 42.
Kadhalika,
umaarufu wa Pinda ambaye anaongoza miongoni mwa wagombea wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), umeshuka kwa asilimia tatu kutoka 12 za mwaka juzi, wakati Zitto
ameendelea na kiwango kilekile cha asilimia tisa alizopata katika utafiti
uliotangulia.
Wengine
wanaofuata na asilimia walizopata kwenye mabano ni Waziri wa Ujenzi, Dk John
Magufuli (8), Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (7) na Mwenyekiti wa CUF,
Profesa Ibrahim Lipumba (5).
Pia wamo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (4) ambaye
amefungana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (4) na Waziri wa Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (2).
Ikilinganishwa
na utafiti wa 2011, Lipumba ameporomoka kwa asilimia tisa.
Lowassa
amepanda kwa asilimia sita, Dk Magufuli asilimia nne, Mbowe na Membe wamepanda
kwa asilimia mbili kila mmoja, wakati Sitta amebaki katika kiwango kilekile cha
asilimia mbili.
Hata hivyo,
utafiti huo umeonyesha kuwa wananchi ambao hawana uamuzi wa kuchagua mtu yeyote
kati ya hao kwa sasa ni asilimia 18, likiwa ni ongezeko la asilimia 12
ikilinganishwa na utafiti uliotangulia.
CCM yatamba.
Katika
utafiti huo, CCM kimeonyesha kuwa ni chama ambacho asilimia 52 ya wananchi
wangependa kujiunga nacho, kikiwa kimepanda chati kwa asilimia moja kutoka
asilimia 51 mwaka jana.
Kwa upande
wa Chadema, wananchi ambao wanapenda kujiunga nacho imeshuka kutoka asilimia 35
mwaka 2011 hadi 31 mwaka jana.
Uwezekano
mkubwa wa CCM kupanda chati ni kutokana na ukweli kuwa mwaka jana kilikuwa na
uchaguzi ulioanzia ngazi ya mashina hadi taifa na kuibua vuguvugu kubwa
masikioni mwa wananchi.
Chadema
hakikuwa na harakati kubwa za kisiasa ukiacha kampeni ya Movement For Change
(M4C), ambayo kwa kiasi haikuwa na pilika kama uchaguzi wa CCM.
Chama
kingine ni CUF ambacho kimeporomoka kwa kupata asilimia 10 mwaka 2011 hadi nne
mwaka 2012.
Hata hivyo,
asilimia ya wananchi kutokutaka kujihusisha na chama chochote imepanda kutoka
asilimia mbili mwaka 2011 hadi 12 mwaka 2012.
Rushwa.
Katika suala
la rushwa nchini, utafiti huo umeonyesha kuwa kati ya watu 10 waliohojiwa,
wanne walikuwa na maoni kuwa rushwa imeongezeka kufikia asilimia 41, asilimia
30 walisema iko palepale, asilimia 23 walisema imepungua na asilimia tano
hawajui.
No comments:
Post a Comment