Radio mbili Radio IMANI na Kwa NEEMA FM zimefungiwa miezi sita, na Clouds FM kupigwa faini ya Shilingi Milioni 5. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, February 26, 2013

Radio mbili Radio IMANI na Kwa NEEMA FM zimefungiwa miezi sita, na Clouds FM kupigwa faini ya Shilingi Milioni 5.


Radio hizi mbili (Radio IMANI na Kwa NEEMA FM ) zimefungiwa miezi sita, na Clouds FM kupigwa faini ya milioni 5.





Radio Kwa NEEMA FM  ya Jijini Mwanza:- Sababu ni kushabikia maswala ya uchinjaji Mwanza.



Radio Iman FM ya Morogoro: Kushabikia watu kutoshiriki Sensa 2012.



Na Radio  Clouds FM ya Jijini Dar es salaa,:-Kuendesha/kushabikia masuala ya ushoga wakati wa uchaguzi wa Marekani, kuendesha kipindi cha uchochezi wakati wa uchaguzi wa Marekani.



-Kuendesha kipengere cha 'Jicho la ng'ombe' kisichofuata maadili.






Makamu Mwenyekiti wa

Kamati ya Maadili ya

Utangazaji nchini,

Walter Bgoya (katikati),

akizungumza na wanahabari

leo jijini Dar es Salaam

ukumbi wa habari Maelezo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo (feb 26,2013)jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Walter Bgoya alisema Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kufuta kipindi chake cha Jicho la Ng'ombe mara moja pamoja na kulipa faini ya sh. milioni 5.



Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kutoanzisha kipindi kingine kinacho fanana na Jicho la Ng'ombe.



Akifafanua zaidi Makamu Mwenyekiti huyo alisema vituo vya Imani FM na Kwa-Neema vimefungiwa kwa kosa la kufanya kazi zao kwa uchochezi jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya tasnia ya utangazaji.




Gari la Kituo cha

Imani FM kilichofungiwa

 likiwa Idara ya Habari Maelezo leo.
 Kituo cha Imani FM kinadaiwa kufanya uchochezi kwa wananchi juu ya suala la sensa ya watu na makazi huku kile cha Kwa-Neema kufanya uchochezi juu ya mgogoro wa uchinjaji wanyama kwa Waislamu na Wakristu mkoani Geita.



Hata hivyo Kamati ya Maadili imeweka mlango wazi kwa vituo hivyo kukata rufaa endapo havikuridhika na adhabu vilivyo pewa kutokana na makosa vinao daiwa kufanya.



Kamati Imevitaka vyombo vyote vya habari kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni Sheria na maadili ya tasnia hiyo ili kuepuka kuzua migogoro kwa wananchi ambao wamekuwa wakiviamini vituo hivyo.



Hata hivyo mara baada ya ujumbe wa kamati hiyo kumaliza kusoma adhabu hizo kwa waandishi wa habari haukuruhusu maswali kwa waandishi wa habari, hivyo waandishi kubaki wameduwaa.





SOURCE: Jamii Forums

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad