Simba SC hoi kwa Mtibwa Sugar yagawa Pointi 6 na kubaki nafasi ya 3 kwa pointi zake 31 lakini hatarini kung’olewa na Coastal Union walio Pointi 1 nyuma . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, February 24, 2013

Simba SC hoi kwa Mtibwa Sugar yagawa Pointi 6 na kubaki nafasi ya 3 kwa pointi zake 31 lakini hatarini kung’olewa na Coastal Union walio Pointi 1 nyuma .




Simba SC  v/s  Mtibwa Sugar 
Beki  Salvatory Ntebe  amefunga bao lake  Dakika ya 16  ya mchezo kati ya Simba SC  dhidi ya  Mtibwa Sugar  na kuwapa ushindi  Mtibwa Sugar na  Kuwafanya sasa Simba SC  wazidi  kupoteza matumaini  ya kutetea Ubingwa wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu wa 2012/2013.


 

Mchezo huo ukichezwa  kwenye  uwanja wa Taifa, Dar es Salaam  umewafanya  Mtibwa Sugar  itimize pointi 27  baada ya kucheza mechi 18 na kupanda hadi nafasi ya 5  kwenye msimamo wa Ligi Kuu  wakati Simba SC  inabaki nafasi ya 3  kwa pointi zake  31  baada ya kucheza mechi 18 pia wakiwa hatarini  kung’olewa na Coastal Union walio Pointi 1 nyuma na Mechi moja mkononi.



Mashabiki wa  Simba SC
Yanga  SC  inaendelea kuongoza ligi hiyo kwa pointi zake 39, ikifuatiwa na Azam  FC  yenye pointi 36.




Simba SC , ambao wanasafiri kwenda  Angola kurudiana na Clube Recreativo de Desportivo do Libolo ambayo ilishinda 1-0 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONS  LIGI, watarudi tena kwenye Ligi kuu  VPL hapo Machi 10 watakapokuwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza na  Coastal  Union.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad