![]() |
Baada
ya matokeo
mabaya
ya
mtihani
wa kidato
cha
nne 2012.
|
Mwenyekiti
wa Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi nchini (TAMONGSCO), Mahmoud
Mringo alisema kwamba maswali waliyoulizwa watahiniwa yalikuwa ya kujieleza
tofauti na miaka ya nyuma, ambapo mfumo uliotumika uliwataka watahiniwa kutaja
vitu tu bila ya kulazimika kuvielezea kwa undani.
![]() |
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dk
Shukuru Kawambwa
|
Kauli yake
iliungwa mkono na Mkuu wa Taaluma katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya
Marian, Florence Mapunda ambaye alisema kuwa mtihani wa mwaka jana ulitaka
zaidi watoto kujieleza tofauti na miaka ya nyuma wakati wanafunzi walipokuwa
wanakariri.
Hata hivyo,
Msemaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), John Nchimbi alisema mfumo wa
mtihani haukubadilika kwa namna yoyote na kuwa upo kama ule wa miaka yote.
Naibu Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo, kwa upande wake alisema madai
yanayotolewa hayana msingi, huku akihoji kwa nini yasitoke tangu mitihani
ilipokuwa ikifanyika na badala yake yanatoka baada ya kutangazwa kwa matokeo.
Matokeo ya
mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana yanaonyesha kuwa watahiniwa
240,903 sawa na asilimia 60.6 wamepata sifuri, huku wanafunzi 23,520 tu ambao
ni sawa na asilimia 5.16 ndiyo waliofaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia
26.02 wamepata daraja la nne.
![]() |
Waziri Mkuu Pinda |
Kutokana na
matokeo hayo, Waziri Mkuu Pinda, juzi alitangaza kuunda tume ya kuchunguza
chanzo cha matokeo hayo kuwa mabaya, hatua ambayo hata hivyo imekosolewa na
wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Tume hiyo
inayoundwa na wajumbe kutoka Taasisi za Elimu, Chama cha Waalimu, Kamati ya
Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania
(Tahossa) inatarajiwa kuanza kazi wiki hii.
Profesa
Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisema kuunda tume ni
kupoteza muda kwa sababu matatizo na changamoto zote ndani ya sekta hiyo
yanajulikana, huku mwenzake, Profesa Chriss Maina pia wa UDSM akisema kuunda
tume hakutaisaidia kwa kuwa Serikali inaidharau sekta ya elimu.
![]() |
Mbatia |
Alisema
matatizo mengine ni mazingira magumu ya kufundisha na uhaba wa walimu.
“Kinachotakiwa wajipange kufanyia kazi changamoto hizi zilizopo badala ya
kuunda tume, wakati fedha nyingi tunasikia inapotea kwenye ubadhirifu,”alisema
Profesa Mpangala.
Naye Profesa
Maina alisema: “Hiyo tume ya kazi gani kwa sababu matatizo yanafahamika wazi,
umewahi kusikia taifa gani ambalo halina mtalaa wa elimu. Hiyo ndiyo hali
halisi kwa nchi yetu. ”
Dk. Slaa
alishangazwa na hatua hiyo ya Waziri Mkuu kuunda tume kwa ajili ya kufuatilia
kufeli kwa wanafunzi, akisema ni juzi tu Bunge limemaliza kikao chake Dodoma na
kuitupilia mbali hoja binafsi ya Mbatia.
Dk. Slaa |
Alisema hoja
binafsi ya Mbatia ilikuwa na nia ya kupitisha azimio la Bunge kuunda kamati
teule ya kuchunguza tatizo la udhaifu katika sekta ya elimu, lakini kwa
ushabiki wa wabunge wa CCM akiwemo Waziri Mkuu, ilikataliwa.
Naye Dk.
Bana alimbeza Pinda kwa hatua hiyo ya kuunda tume kwa masuala ya mtihani,
akisema tatizo la kufeli kwa wanafunzi halihitaji tume kwani kasoro ziko wazi.
Alisema kuwa
matatizo ya walimu yanajulikana, huku serikali ikijidanganya kutengeneza sera
ya elimu kinyemela bila kushirikisha wataalamu.
ALAMA ZA
JUMLA ZA UFAULU WA MTIHANI WA TAIFA KIDATO CHA NNE 2012.
Div 1 =1,641.
Div 2 =6,453.
Div 3 =15,426.
Div
4 =103,327.
Div
0 =243,903.
Habari Na:Mwananchi.
No comments:
Post a Comment