Cheki Matokeo ya Ligi Soka Mbalimbali za Ulaya huku Manchester City , Real Madrid,FC Barcelona na Bayern Munich wakipa Pointi 3 Muhimu katika Michezo yao. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, February 24, 2013

Cheki Matokeo ya Ligi Soka Mbalimbali za Ulaya huku Manchester City , Real Madrid,FC Barcelona na Bayern Munich wakipa Pointi 3 Muhimu katika Michezo yao.


Manchester City
Mabingwa  watetezi wa  Ligi kuu Soka nchini Uingereza  Manchester City  wakicheza  nyumbani  uwanja wa Etihad, leo (Feb 24,2013) wameichapa Chelsea  bao 2 - 0  na  kujiimarisha  nafasi ya pili  ya Msimamo wa Ligi hiyo  na kuzidi   kuwasogelea Vinara wa Ligi Manchester  United  kwa kuwa Pointi 12 nyuma yao Mechi zikiwa zimebaki 11  lakini  Chelsea sasa wapo hatarini kwenye  4 bora kwani wako nafasi ya 3 na nyuma yao kwa Pointi 1 tu ni Tottenham walio na Mechi 1 mkononi na wanafuatia Arsenal walio nafasi ya  5  Pointi 2 nyuma ya Tottenham.


 

Katika mchezo Mwingine: Newcastle walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuishinda Southampton, iliyo nafasi za hatari za kushushwa Daraja, Bao 4-2 katika Mechi iliyochezwa St James Park.



Ushindi huu umeipandisha Newcastle nafasi kadhaa katika Msimamo wa Ligi Kuu England na sasa wapo nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 30 zikiwa ni Pointi ni Pointi 6 juu ya zile Timu 3 za mkiani ambayo ni sehemu ya hatari kwani ni eneo la kuporomoka Daraja mwishoni mwa Msimu.



MSIMAMO.


1 . Manchester   United  Pointi 68


2 . Manchester   City  Pointi  56


3 . Chelsea  Pointi   49


4 . Tottenham  Pointi  48


5 . Arsenal  Pointi  47


6 . Everton  Pointi  42
 

7 . WBA  Pointi  37


9 . Liverpool  Pointi  39




Real Madrid
Huko nchini Hispania  katika  La Liga: FC Barcelona walizidi  kujiimarisha na kuwa na nafasi nzuri ya kutwaa  Ubingwa  baada ya kuichapa Sevilla kwa Bao 2-1 hii ikiwa ni Mechi yao ya kwanza toka wapokee kichapo kule San Siri  mikononi  mwa AC Milan  katika  mashindano ya  UEFA .



Sevilla ndio waliotangulia kufunga kwa Bao la Botid   Dakika ya 42, na Barca kusawazisha Dakika ya 51, kwa Bao la David Villa, na Lionel Messi kufunga Bao la pili, Dakika ya 60.



Nao Mabingwa  watetezi Real Madrid na ushindi  wa  bao  2  za kipindi cha Pili ,kupitia kwa Wachezaji wao  Gonzalo  Higuain na Kaka, zimewapa ushindi   wa ugenini dhidi ya Deportivo  La Coruna.



Deportivo ndio waliotangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 34 la Riki na Real kupiga Bao Dakika ya 73, Mfungaji Kaka, na Dakika ya 88 la Higuain.



Katika mchezo huo  Winga wa Real  Angelo Di Maria  alitolewa kwa Kadi Nyekundu Dakika ya 90 kufuatia Kadi za Njano mbili mfululizo.



MSIMAMO


1 Barcelona  Pointi   68


2 Atletico Madrid  Pointi  53


3 Real Madrid  Pointi   52


4 Malaga   Pointi 42


5 Valencia   Pointi  41


6 Real Sociedad  Pointi  40




Borussia Dortmund
Kwenye Ligi ya Ujerumani : Bundesliga  Vinara   Bayern Munich  waliifumua Werder Bremen  Bao 6-1 na kujichimbia kileleni  wakiwa Pointi 18 mbele ya Mabingwa  Borussia Dortmund  ambao leo (Feb 24,2013 )wanacheza ugenini  na  Borussia Mönchengladbach.



MSIMAMO


 1 . Bayern Munich   Pointi 60


2 . Borussia Dortmund   Pointi 42


3 . Bayer Leverkusen   Pointi 41


4 . Eintracht Frankfurt  Pointi  38


5 . Freiburg  Pointi  35


6 . Hamburger  Pointi  34


7 . Hannover  Pointi  33


8 . Mainz  Pointi  32




AC Milan
Aidha  AC Milan  Jumapili  hii  wana kibarua kipya kwenye Serie A watakapocheza Dabi ya Jiji la Milano na Mahasimu wao wakubwa Inter Milan  katika uwanja wa  San Siro, Uwanja ambao kwa Mahasimu hao wote wawili ndio Nyumbani, huku AC Milan wakikamata nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 44 na Inter wapo nafasi ya 5 wakiwa na Pointi 43.



MSIMAMO



1 Juventus  Pointi  55


2 Napoli   Pointi  51


3 AC Milan  Pointi  44


4 Lazio  Pointi   44


5 Inter Milan  Pointi  43


6 Fiorentina  Pointi   42


7 Catania   Pointi   39

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad