Tanzania
imetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi
zinazokabiliwa na tatizo la rushwa ndani ya jeshi.
Taasisi ya Transparency International (TI), ambayo hutafiti masuala ya rushwa duniani imeitaja Tanzania kwamba jeshi lake lina rushwa kubwa na ndogondogo.
Kwa
mujibu wa gazeti dada la The Citizen la jana Jumapili, uongozi wa Jeshi la
Wananchi Tanzania (JWTZ) umekanusha vikali taarifa ya taasisi hiyo.
TI
inadai katika taarifa yake kuwa sekta ya ulinzi ya Tanzania inakabiliwa na
tatizo hilo na hiyo ni kutokana na mambo yake kuendeshwa kwa usiri mkubwa.
“Hakuna
kitu kibaya kama la rushwa kwenye jeshi, maana kuna fedha nyingi inatembea
kutokana na ughali wa vifaa vya kijeshi.
Bado
Serikali nyingi zinafanya mambo haya kuwa siri na kutoa mwanya kwa rushwa kutembea.
“Fedha inayotumika vibaya kwa masuala ya kijeshi, ingeweza kutumia vizuri zaidi katika masuala ya maendeleo,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo iliyoandikwa na Mark Pyman, ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha masuala ya Ulinzi cha Transperancy International.
Transparency
International inaeleza kuwa fedha ya
rushwa inayotembea kwenye sekta ya ulinzi inakadiriwa kufikia kiasi cha Dola 20
bilioni (Sh32 trilioni).
“Ripoti
ya Transparency International itufungue macho Watanzania maana kwa kawaida huwa
kila watu wakihoji mapato na matumizi ya jeshi tunaambiwa hatuwezi kujibiwa kwa
madai ya woga wa kuhatarisha usalama wa taifa,” alikaririwa mbunge mmoja na
gazeti la The Citizen.
Tanzania,
hata hivyo, iko juu ya nchi nyingi za Afrika kwa tatizo la rushwa ingawa inatakiwa
kurekebisha mianya mingi kwenye sekta hiyo.
“Tunaona
Tanzania ina changamoto ya kuimarisha vyombo vya kutupa jicho kwenye jeshi.
Mathalani, kuna Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Mambo ya Nje, lakini haina meno ya
kuingia kwa undani masuala ya kijeshi,” iliongeza Transparency International.
Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe, hata hivyo, alikaririwa na gazeti la The Citizen akidai kuwa taasisi yake imekuwa ikifanya kazi kitaalamu na kimaadili akitolea mfano jinsi wanavyoajiri wanajeshi kwa kufuata vigezo.
Transparency
International inasema kuwa kuna Kitengo cha Utawala Bora cha Serikali ambacho
hufanya ukaguzi kwenye jeshi ingawa halijatoa ripoti ya aina yoyote kuhusiana
na ukaguzi wa bajeti ya jeshi.
“Mfano
kuna taarifa kuwa Kitengo cha Kilimo cha Jeshi la Kujenga Taifa (Suma-JKT) kuna
kinajishughulisha na uchimbaji madini na biashara nyingine lakini kuna udhibiti
mdogo,” iliongeza taarifa yao.
Julai
mwaka jana, maofisa saba waandamizi wa Bodi ya Zabuni ya Suma-JKT walifunguliwa
mashitaka ya matumizi mabaya ya ofisi na uhamishaji usio wa halali wa zaidi ya
Sh 3.8 bilioni.
Waliotuhumiwa ni pamoja na Kanali Ayoub Mwakang’ata, Luteni Kanali Mkohi Kichogo, Luteni Kanali Paul Mayavi, Meja Peter Lushika, Sajini John Laizer, Meja Yohana Nyuchi na Luteni Kanali Felix Samillan wanaodaiwa kufanya makosa hayo mwaka 2009.
Tanzania
imewekwa katika Kundi D kwenye orodha hiyo ya Transperancy International ya
nchi zinazokabiliwa na kiwango cha juu cha rushwa na vigezo vinavyoangaliwa ni
sekta za siasa, fedha, utumishi wa Kundi la D ni nchi ambazo zinakabiliwa na
kiwango cha juu cha rushwa na katika orodha hiyo zimo pia nchi za Russia na
China.
Hata
hivyo, nchi zenye kiwango cha juu cha rushwa ziko katika Kundi F wakati zile
zenye kiwango cha chini cha rushwa ziko Kundi A.
Chanzo:Mwananchi
No comments:
Post a Comment