![]() |
Beautiful
Onyinye,
Wema
Isaac Sepetu
akiwa
ofisini kwake.
|
Wakati Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu akionesha
jeuri ya fedha kwa kufungua bonge la ofisi ya kuzalisha filamu, zilipendwa
wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemjibu kwa kukamilisha mjengo wa maana
uliogharimu Sh. milioni 260 hivyo kwa pamoja kuthibisha msemo kuwa fedha
inaongea, Ijumaa Wikienda lina data kamili.
Katika
uzinduzi huo ambao Ijumaa Wikienda lilialikwa, Wema ndiye alikuwa wa kwanza
kumshtua mama yake mzazi, Mariam Sepetu na mastaa mbalimbali (akiwamo Diamond),
Jumatano iliyopita na kuzindua ofisi yake inayojulikana kwa jina la Endless
Fame Films iliyopo Mwananyamala- Komakoma, jijini Dar.
![]() |
Beautiful
Onyinye,
Wema
Isaac Sepetu
akiwa
ofisini kwake.
|
Pamoja na
mkali huyo ambaye ni sura ya mauzo kwenye gemu la filamu za Kibongo kumualika
mama yake, ilibainika kuwa hakuwa amemtaarifu kabla kuhusu umiliki wa ofisi
hiyo hivyo ilikuwa ‘sapraizi’ kwa mzazi huyo.
“Mama hii
ndiyo ofisi yangu ambayo maandalizi yake yalianza tangu Juni, mwaka jana na
sikutaka kukwambia hadi ilipokamilika ili iwe sapraizi,” Wema alimwambia mama yake mbele ya wageni
waalikwa na kuongeza:
“Nia na
madhumuni ya ofisi hii ni kukuza vipaji vya wasanii wachanga hivyo nakaribisha
chipukizi wa filamu waje kujiunga kwenye kampuni yangu.”
Bila kutaja
gharama za ofisi hiyo, Wema alisema kwa kifupi kuwa imemgharimu mamilioni ya
shilingi huku akiainisha vitu vilivyosheheni ndani kama jiko, ofisi yake,
sehemu ya kunywea kahawa, kupumzikia wageni, vyumba viwili vya wahariri wa
video pamoja na choo cha ndani.
![]() |
Mjengo wa
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ unaoendelea kujengwa ambao utagharimu Sh.
milioni 260.
|
![]() |
Gari la
Diamond likiwa limepaki nje ya mjengo wake.
|
Siku hiyo
ilipambwa na mastaa mbalimbali wa filamu kwa ajili ya kumpa sapoti mwenzao
(Wema) ambaye ameonesha kupiga hatua kubwa kwenye sanaa wakiongozwa na Vincent
Kigosi ‘Ray’, Jacob Steven ‘JB’, Single Mtambalike ’Richie’, Issa Mussa
‘Cloud’, Hartman Mbilinyi na Husna Posh ‘Dotnata’.
Wakati
mastaa waliofika kwenye sherehe hiyo ya Wema wakijiuliza juu ya kutohudhuria
kwa Diamond, taarifa zilizonaswa na gazeti hili zilidai kuwa alikuwa katika
mishemishe za kumjibu Wema kwa kuzindua mjengo wake wa kisasa uliopo Tegeta,
jijini Dar.
Akizungumza
na paparazi wetu akiwa kwenye eneo ilipo nyumba hiyo ambayo ilikuwa ikifanyiwa
‘finishing’, Diamond alisema kuwa nyumba hiyo yenye thamani ya Sh. milioni 260
ni zawadi kwa mama yake Sanura Kassim ‘Sandra’.
“Mama yangu
ndiyo kila kitu kwangu, mara ya kwanza nilimnunulia gari aina ya Toyota Alteeza
nikaona haitoshi, nikaamua kumjengea hii nyumba ambayo itakuwa kama urithi wake
hata nikifa leo,” alisema Diamond.
Diamond
alimzungusha paparazi wetu na kujionea mjengo huo wenye vyumba vinne vya kulala
ambavyo vyote ni ‘self contained’ (chumba chenye choo na bafu), studio kubwa ya
kurekodi muziki, eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya kujenga bwawa la kuogelea
‘swimming pool’, uwanja wa basketball na sehemu maalum ya kufanyia mazoezi
(gym) ambapo alisema hadi ifikapo Septemba, mwaka huu kila kitu kitakuwa
kimekamilika.
Ukiachana na
ukubwa wa nyumba hiyo, uwanja ambao ameuzungushia uzio wa ukuta kuna nyumba
nyingine ndogondogo tatu ambazo kwa mujibu wa staa huyo wa Songi la Kesho, zitakuwa
zikipangishwa.
Stori Na :
Shakoor Jongo na Imelda Mtema
No comments:
Post a Comment