Inter Milan yapigwa faini ya Euro 50,000 na Kamati ya nidhamu ya Ligi Kuu nchini Italia maarufu kama Serie A kisa vitendo vya kibaguzi kwa Mario Balotelli. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, February 26, 2013

Inter Milan yapigwa faini ya Euro 50,000 na Kamati ya nidhamu ya Ligi Kuu nchini Italia maarufu kama Serie A kisa vitendo vya kibaguzi kwa Mario Balotelli.

Mario Balotelli.
Kamati  ya nidhamu ya Ligi Kuu nchini Italia maarufu kama Serie A limeitoza faini ya Euro 50,000  klabu ya Inter Milan baada ya mashabiki wake kukutwa na hatia ya kumfanyia vitendo vya kibaguzi mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo Mario Balotelli. 


 


Tukio lilitokea wakati Balotelli akiichezea kabla yake mpya ya AC Milan katika mchezo dhidi ya Inter ambao ulimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1. 



Mashabiki wa Inter Milan  walikuwa wakipeperusha maganda ya ndizi katika mchezo huo lakini baadhi wachambuzi walidai pengine tukio hilo halikumlenga nyota huyo ambaye ameitumikia klabu hiyo kwa miaka minne. 



Balotelli ambaye ametokea Manchester City kabla ya kwenda AC Milan naye pia metozwa euro 10,000 kwa kuwaonyesha ishara ya matusi mashabiki hao. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad