Nyumba hizo
zilijengwa katika Mtaa wa Vikongoro, Kata ya Chanika Wilaya ya Ilala katika eneo ambalo linadaiwa
kuwa na Mgogoro.
Akisimulia
tukio hilo, mkazi wa kitongoji hicho, aliyejitambulisha kwa jina la Yusuph
Kondo (80) alisema mchana wa jana alimwona Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa akiwa na
kidumu cha mafuta na kwamba alielekea kwenye nyumba ya Zaituni Mguguli
na mara baada ya kufika eneo hilo aliona moto ukiunguza nyumba.
Naye mtoto
wa Zaituni aitwaye Ajuaye Twaha(10), alisema walifika mwenyekiti akiwa na
askari na kumwamuru atoke nje na kwamba
alimuona askari akimwagia mafuta na kuwasha moto.
Akizungumza
kwa masikitiko, Zaituni alisema samani za ndani, magodoro na Sh 900,000
alizopewa na mtoto wake wa kwanza ili
kumlipia ada mdogo wake ziliungua ndani ya nyumba hiyo.
Miongoni mwa
wakazi waliopata hasara kutokana na
tukio la kuungua nyumba zao, ni Fikiri Hassan, Zuberi Kiiba, Asha
Abdallah, na Issa Salehe.
Ofisa
Mtendaji wa mtaa huo, Ali Kambi, alipoulizwa juu ya tukio hilo alikiri na kwamba lilitokana na mgogoro wa ardhi.
Alisema
waliochomewa nyumba wote walivamia eneo la mtu anayeitwa Nicolaus Malose
aliyemilikishwa na kijiji tangu 2011.
Hata hivyo
waathirika wa tukio hilo walisema eneo hilo ni lao tangu mwaka 1985.
Mkuu wa
Kanda ya Kipolisi Ilala, Marietha Minongi
Komba alipoulizwa jana kuhusu tukio hilo
alisema hakuwa na taarifa za kuungua kwa nyumba na kwamba siku ya jana
alizungumza na Mkuu wa Kituo cha Polisi Ukonga mara saba, lakini
hakupata taarifa zozote.
No comments:
Post a Comment