 |
Basi la
Bunda lililokua linatokea Musoma kwenda Mwanza limepata ajali nje kidogo ya
Magu eneo la katikati ya Kahangalala na Ihayabuyaga na watu watatu wanahofiwa
kufariki katika ajali hiyo na zaidi ya 10 kujeruhiwa.
|
 |
Mazingira
yanaonesha kuwa idadi kubwa ya watu wamejeruhiwa na hofu kubwa imetanda eneo la
tukio kuhofia usalama wa hali za abiria waliomo ndani ya basi husika kwani basi
limepinduka tairi zikielekea juu, limetumbukia kwenye majaruba ya mpunga,
limepondeka vibaya upande mmoja.
|
 |
Hakuna pa
kujisitiri kwa watoto hawa ambao walikuwa wakisubiri wazazi wao kuokolewa toka
ndani ya basi hilo zaidi ya kujisitiri kwa kanga, vitenge na mashuka
waliyoambulia toka kwenye baadhi ya mabegi yao.
|
 |
Hali ya
baadhi ya barabara za ndani zinazounganisha vijiji wilayani Magu zimefunikwa na
maji na hii ndio Barabara na hali ya hewa na mazingira.
|
 |
Baadhi ya
nyumba zilizo karibu na eneo la ajali nazo zimeathiriwa na mvua kubwa
inayoendelea kunyesha eneo hili wilayani Magu.
|
 |
Hali ya
uokoaji imeathiriwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha eneo hili ni wachache
tu abiria wameweza kupewa miamvuli na watu walio kwenye magari yanayopita eneo
hili ili wapate kujisitiri.
|
PICHA KWA
HISANI YA GSENGO
No comments:
Post a Comment