Hayo
yalielezwa na daktari bingwa wa uchunguzi wa magonjwa katika Kitengo cha
Patholojia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk Henry Mwakyoma na Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Saratani katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk
Crispin Kahesa.
Madaktari
hao wametaja mambo mengine yanayoweza kusababisha saratani ya shingo ya kizazi
kuwa ni kujiingiza kwenye mapenzi katika umri mdogo, kuolewa mara nyingi, kuwa
na wapenzi wengi, kusafisha sehemu za siri kwa bidhaa zenye kemikali na kuzaa
mara nyingi.
Katika
kiwango cha kimataifa, wastani wa mwanamke kuzaa bila kuwa katika hatari ya
kupata ugonjwa wa saratani, ni watoto wanne.
Dk Mwakyoma
alisema saratani ya shingo ya kizazi inatokana na aina 40 ya virusi, aina mbili
ikiwa ni virusi vinavyosambaa kwa njia ya ngono... “Human papilloma virus (HPV)
Squamos cell carcinoma kirusi namba 16 na Adenocarcinoma namba 18, ni kati ya
virusi 40 vinavyosababisha saratani ya kizazi na vyenyewe vinachangia tatizo
hilo kwa asilimia 70.”
Alisema
saratani ya uzazi ndiyo inayoongoza ikilinganishwa na nyingine nchini na
asilimia 80 ya wagonjwa, wameambukizwa kwa ngono.
“Saratani
hiyo husambaa kwa ngono kutoka mwanamke mmoja kwenda kwa mwingine.
Mwanamke
mwenye saratani ya kizazi akifanya ngono, mwanamume huchukua virusi na
kumwambukiza mwingine atakayefanya naye ngono,” alisema na kuongeza.
“Wagonjwa
wengi na wale ambao tayari wana maambukizi, wamekuwa wakikutwa na virusi hawa
wa aina mbili ambao wamekuwa wakienezwa zaidi kwa njia ya zinaa.
Inawezekana
mwanamume akawa ametoa kirusi kwa mwanamke mmoja kwenda kwa mwingine.”
“Hata hivyo,
kuna wanaume ambao tayari wameshakuwa na maambukizi ya HPV wanatembea na
virusi, hawa tunawaita (high risk sexual male patner) wanaume hawa utakuta kila
akioa mke anakufa kwa saratani ya shingo ya uzazi, lakini kamwe virusi hao
hawawezi kumwathiri yeye.”
Alisema
kuanza ngono mapema nako kunachangia kwa kiasi kikubwa maambukizi ya saratani
hiyo, kwani binti anakuwa katika hatari zaidi ya kupata maambukizi mapema na
hivyo kuweza kumwathiri mapema zaidi, tofauti na yule aliyeanza baadaye.
“Idadi kubwa
ya wanawake wamekutwa na saratani mapema sana, ukilinganisha na umri wao,
lakini wengi wao wamekuwa wakikutwa na ugonjwa huu kuanzia umri wa miaka 35
kwenda juu.
Hii
inamaanisha kuwa walipata maambukizi hayo walipokuwa na miaka 20-25.”
Dk Mwakyoma
alisema licha ya hivyo mgonjwa anaweza asitambue tatizo hilo mpaka miaka 10
hadi 15 baadaye ambapo tatizo linajitokeza hadharani.
Chanzo:
Mwananchi.
No comments:
Post a Comment