![]() |
Uganda (The Cranes) |
Kwa kutwaa
kombe hilo, ambalo ni la nne kwa kocha wao Bobby Williamson, Uganda imeondoka
na zawadi ya kwanza ya kombe na dola 30,000 wakati Wakenya walioshina nafasi ya
pili wamepata dola 20,000 huku Zanzibar Heroes iliyoshika nafasi ya tatu imepata
dola 10,000.
![]() |
Mrisho Ngassa |
Nyota wa
Uganda, Brian Umony ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Michuano hiyo na tuzo ya
kipa bora imekwenda kwa kipa wa Uganda, Hamza Muwonge, ambaye ameruhusu goli
moja tu katika michuano yote, ambapo Uganda wameshinda mechi zao zote.
Utata
umekuja katika tuzo ya mfungaji bora baada ya kupewa Robert Ssentongo wa
Uganda, mwenye magoli manne na kuachwa Mrisho Ngassa na John Bocco waliofunga
magoli matano kila mmoja.
WAFUNGAJI
CECAFA TUSKER CHALLENGE 2012.
John
Bocco Tanzania 5
Mrisho
Ngassa Tanzania 5
Robert
Ssentongo Uganda 4
Brian
Umony Uganda 3
Khamis
Mcha Zanzibar 3
Suleiman
Ndikumana Burundi 3 (1 penalti)
Chris
Nduwarugira Burundi 3
Geoffrey
Kizito Uganda 2
David
Ochieng Kenya 2
Clifton
Miheso Kenya 2
Dadi
Birori Rwanda 2
Mike
Barasa Kenya 2
Rais wa
CECAFA, Leodegar Tenga alikuwapo jukwaani kuwakabidhi zawadi washindi.
![]() |
Zanzibar Heroes |
Zanzibar
Heroes ilipata ushindi wa tatu baada ya kuwafunga ndugu zao wa Tanzania Bara
kwa penalti 6-5, baada ya dakika 90 za mechi yao kumalizika kwa sare ya 1-1.
Tanzania
Bara walihitaji kukaza kwa dakika nne tu za mwisho ili kupata ushindi wa 1-0
kupitia goli la mapema dakika ya 10 lililofungwa na Mwinyi Kazimoto kufuatia
pasi ya kichwa ya John Bocco.
Lakini
mchezaji Abdallah Othman Ali aliyeingia akitokea benchi kuchukua nafasi ya
kiungo Suleyman Kassim 'Selembe', aliisawazishia Zanzibar goli katika dakika ya
86.
![]() |
Kocha Mkuu
wa Zanzibar, Salum Nassor Bausi akiwa amebebwa na wachezaji wake kwa furaha
|
Sabri Ali
Makame ndiye aliyefunga penalti iliyowapa ushindi Zanzibar baada ya beki Kelvin
Yondani kupiga nje penalti yake wakati wa kupigiana penalti moja-moja baada ya
tano za kwanza kumalizika huku kila timu ikiwa imefunga nyingine moja-moja ya
hatua hiyo ya "piga nikupige".
Katika
penalti tano-tano za kwanza kila timu ilikosa penalti moja. Mwinyi Kazimoto
alikosa penalti ya nne kwa upande wa Bara iliyodakwa na kipa wa Zanzibar wakati
Nasoro Masoud "Chollo" alikosa penalti ya nne ya Zanzibar Heroes
iliyodakwa na kipa wa Bara, Juma Kaseja.
Waliopata
penalti zao kwa upande wa Bara walikuwa Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shabani
Nditi, Shomary Kapombe na Frank Domayo, wakati waliofunga kwa upande wa
Zanzibar walikuwa ni Khamis Mcha, Samih
Nuhu, Aggrey Morris, Abdallah Othman Ali, Nadir Haroub 'Cannavaro', na Sabri
Ali Makame aliyepiga ya ushindi.
No comments:
Post a Comment