![]() |
Gari
aina ya Land Cruiser
mali
ya chuo cha SUA
cha
mjini Morogoro
kama
linavyoonekana
baada
ya kupigwa mawe
na
watu wanaodhaniwa
kuwa
ni majambazi
nje
kidogo ya mji wa Singida.
|
Watu wasiofahamika idadi yao na ambao wanadhaniwa kuwa ni
majambazi, wamevamia gari lililokuwa linasafirisha maiti kutoka Morogoro mjini
hadi mkoa wa Mara na kupora zaidi ya
shilingi milioni 19.8.
Baada ya kumaliza zoezi la uporaji huo, majambazi hayo
yalishusha jeneza na kisha kulifumua na kuanza kulisachi.
Jeneza hilo lilikuwa limebeba mwili wa mwanafunzi Munchari Lyoba, mwanafunzi wa mwaka wa tatu
aliyekuwa anasomea elimu ya biashara kwenye chuo cha SUA.
Amesema gari hilo lilibeba viongozi wa wanafunzi sita na
viongozi wengine wanne akiwemo dereva.
![]() |
Land Cruiser namba SU 37012 |
Akizungumza na waandishi wa habari leo nje ya chumba cha
kuhifadhi maiti cha hospitali ya mkoa wa Singida, mkuu wa msafara huo
Makarang Nouna, amesema tukio hilo
limetokea Disemba 6 mwaka huu saa 7.30 usiku, na lilihusisha gari Land Curise
lenye namba za usajili SU 37012 na lilikuwa likiendeshwa na Kalistus Malipula.
Amesema tukio hilo la kinyamana la kusikitisha, limetokea katika barabara kuu ya Dodoma –
Mwanza nje kidogo ya mji wa Singida kwenye kona maarufu kwa jina la Mohammed
Trans.
Amesema walipofika eneo la tukio, walikuta mawe makubwa
yamepangwa kukatisha barabara, kitendo kilichosababisha washindwe kupita, na
hivyo kutoa mwanya kuvamiwa na kundi kubwa la vijana ambao walibeba bunduki
mbili aina ya gobore, marungu, mashoka na mawe.
Makaranga amesema walichofanya kwanza ni kupiga kioo cha gari
letu kwa mbele, na baadaye kumparaza kwa panga usoni dereva wetu Kalistus
Malipula.
Baada ya hapo walivunja vunja vyoo vyote na kutuamuru kutoa
kila kitu ambacho tulikuwa nacho.
Akifafanua zaidi, amesema kwa upande wake yeye ameporwa shilingi milioni mbili ambazo
zilikuwa kwa ajili ya kugharamia msafara huo, jumla ya shilingi milioni 8.8
ambazo zilichangwa na wanafunzi kama
rambi rambi kwa mwenzao, na shilingi
milioni tisa ambazo wasindikizaji walikuwa nazo zikiwa ni posho.
“Pia tumeporwa simu
zetu zote za mikononi, viatu,
laptop na mabegi yote ya nguo zetu”amesema.
Makaranga ambaye amesema anafanya kazi za kiutawala katika
chuo cha SUA, amewataja walioumizwa zaidi ni pamoja nay eye, dereva Malipula na
kiongozi wa wanafunzsi Idd Idd na kutibiwa katika hospitali ya mkoa na
kuruhusiwa.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen
Mlozi, ambaye aliwasiliana na uongozi wa SUA Morogoro kwa ajili ya shughuli ya
kutuma gari jingine na ukarabati wa jeneza, amesema kuwa kwa ushirikiano wa
jeshi la polisi na kamati ya ulinzi na usalama, watahakikisha watu waliofanya
unyama huo, wanakamatwa mapema iwezekanavyo ili waweze kufikishwa mbele ya
vyombo vya sheria.
No comments:
Post a Comment