![]() |
Zao la Pamba. |
Ukuaji huo
wa asilimia 7.1 unatokana na ongezeko la uzalishaji katika shughuli mbalimbali
za kiuchumi zikiwemo za kilimo, Uvuvi, Viwanda, Ujenzi na zile za utoaji wa
huduma mbalimbali za jamii.
Akitoa
taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi
ya Taifa ya Takwimu, Morrice Oyuke
amesema kuwa lengo la utoaji wa
taarifa hizo kwa vipindi vifupi vya vya
robo mwaka unalenga kuwapatia wadau wa Takwimu za Pato la Taifa uwezo wa
kutathmini mabadiliko ya ukuaji wa uchumi nchini.
Amesema kuwa
jumla ya thamani ya pato la Taifa katika kipindi cha robo ya mwaka 2012 ni
shilingi 4,220,535 milioni ikilinganishwa na kiasi cha shilingi milioni
3,940,261 za mwaka 2011.
Amefafanua
kuwa ukuaji wa shughuli uzalishaji katika shughuli za kilimo nchini ulifikia
asilimia 1.4 katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2012 zikilinganishwa na
asilimia 1.2 katika kipindi hicho kwa mwaka 2011 kutokana na upatikanaji wa
mvua za kutosha nchini katika mikoa inayozalisha mazao kwa wingi.
![]() |
Samaki aina ya Sangara. |
Amesema ukuaji katika shughuli za uvuvi
ulikua asilimia 2.6 katika robo ya
kwanza ya mwaka 2012 huku shughuli za uchumi katika sekta ya viwanda na Ujenzi
ambayo inahusisha uchimbaji wa madini na kokoto ikikua kwa asilimia 14.3 ikilinganishwa
na 0.8% za mwaka 2011.
Oyuke
ameongeza kuwa ongezeko hilo la
uzalishaji wa madini ya dhahabu linatokana na uzalishaji wa wa madini ya
dhahabu kutoka kilo 8,140 kwa mwaka 2011 hadi kufikia kilo 16,736 kwa mwaka
2012.
Pia
amebainisha kuwa shughuli za utoaji wa
huduma za biashara za jumla na rejareja, ukarabati wa magari na pikipiki na
vifaa vingine vya majumbani katika kipindi hicho zilifikia asilimia 9.0 huku
shughuli za upangishaji nyumba na biashara zikiwa 8.2 %, uchukuzi na
mawasiliano 16.4%, hoteli na migahawa 3.8%, Benki asilimia 15 shughuli za
uendeshaji serikali 6.4%, Elimu 6.1% na
utoaji wa huduma za Afya nchini zikikua kwa kasi ya asilimia 5.1.
No comments:
Post a Comment