![]() |
Francis Cheka |
Shirilisho
la Ngumi la Kimataifa (IBF) limepongeza bingwa mpya wa uzito wa Super Middle
katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki yaa Kati, Mtanzania Francis
Cheka.
Katika barua
yake aliyomtumia Francis Cheka ya tarehe 28/12/2012 Mwenyekiti wa kamati ya
Ubingwa wa IBF/USBA Lindsey Tucker alisema “Tunachukua fursa hii kukutakia
maisha na mafanikio mazuri kama bingwa wa IBF na kumhimiza kuishi kama bingwa”.
Cheka
atatakiwa kutetea taji lake katika kipindi cha miezi sita kufikia mwezi wa 6
mwakani dhidi ya mpinzani ambaye ana rekodi ya mapambano yasiyopungua 15 na
mengi awe ameyashinda hususan mapambano mawili ya mwisho.
Aidha Bondia
Francis Cheka alimaliza mwaka vizuri baada ya kuibuka na ushindi wa pointi
80-75 dhidi ya bondia kutoka Malawi, Chiotra Chimwemwe katika pambano lao hilo
kali la kimataifa la uzito wa Super
Middle katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki yaa Kati
lililofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha juzi.
Chimwemwe
ambaye alitajwa kuwa ni mwanajeshi wa cheo cha luteni usu nchini kwao Malawi,
alionyesha ushindani mkali lakini hadi kufikia raundi ya 12, ni Cheka ndiye
aliyeibuka kidedea baada ya majaji kumpa ushindi wa pointi 80-75.
Matokeo hayo
yalimfanya Cheka aendeleze vipigo kwa kila bondia aliyekutana naye na hivyo
kumaliza vyema mapambano yake mwaka huu.
Akizungumza
mara baada ya pambano hilo, Cheka alisema kuwa amefurahi kwani mpinzani wake
alionyesha umahiri mkubwa.
Chimwemwe alikubaliana na matokeo na
kumpongeza Cheka
No comments:
Post a Comment