Makosa hayo
yaliyotokea yalibainishwa na kamanda wa
jeshi la polisi mkoani Kagera Philip Kalangi (kushoto) kwenye taarifa yake
aliyoitoa mbele ya katibu tawala wa mkoa wa Kagera Nassor Mnambila wakati
maadhimisho ya kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika kwenye viwanja vya
uhuru vilivyoko katika manispaa ya Bukoba.
Kwenye
taarifa hiyo Kalangi aliyataja makosa ya ukatili wa kijinsia kuwa ni pamoja na
306 ya ubakaji, 12 ya kulawiti, 135 ya shambulio na kipigo, 18 ya kutorosha
wanafunzi, 96 ya kutelekeza familia, 20 dhidi ya ukatili wa watoto na 25 ya
mimba kwa wanafunzi.
Alisema
katika kipindi hicho kesi za makosa ya ukatili wa kijinsia 170 zilifikishwa mahakamani ,
aliendelea kusema kuwakesi za makosa 56
bado ziko kwenye upelelezi, kesi za makosa 50 zilipata mafanikio na kesi za
makosa 80 zilikosa mafanikio.
Kushoto ni
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera, Philip Kalangi na katibu tawala wa mkoa wa Kagera Ndg Nassor Mnambila.
|
Kalangi
alisema jeshi la polisi mkoani Kagera litahakikisha linaimarisha amani na
utulivu na maendeleo kwa kuchukua hatua mbalimbali dhidi ya wale wote
wanaofanya vitendo viovu kwa kushirikiana na wadau wengine wa usalama chini ya
dawati la jinsia la jeshi la polisi.
Aliendelea
kusema kuwa ukatili na unyanyasaji wa kijinsia ni uharifu kama uharifu mwingine
wowote, “jeshi la polisi halitamwonea aibu mtu yotote atakayejihusisha na
masuala ya kutekeleza masuala ya ukatili ya kijinsia, tutamshughulikia bila
kujali cheo chake, rangi yake na nafasi yake aliyonayo ndani ya jamii” alisema.
Katibu
tawala wa mkoa wa Kagera Nassor Mnambila aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa
maadhimisho hayo alilipongeza jeshi la polisi mkoani humo kwa juhudi
linalozifanya za kupambana na vitendo vya uharifu mkoani Kagera.
Alilitaka
jeshi hilo lisilegeze kamba badala yake liwashughulikie kikamilifu wale wote
wanaijuhusisha na vitendo vunavyohatarisha amani na utulivu ndani ya jamii,
alisema serikali mkoani Kagera itaendelea kuliunga mkono jeshi hilo ili
likamilishe adhima yake ya kuthibiti kabisa vitendo vya uharifu mkoani Kagera.
No comments:
Post a Comment