Cheki Video ya Mchezaji Lionel Messi akiifungia Timu yake Barcelona na kuvunja Rekodi ya tangu Mwaka 1972 ya Straika wa Ujerumani Gerd Muller ya kufunga Bao 85 ndani ya Mwaka mmoja wa Kalenda kwa yeye kufikisha Mabao 86. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, December 11, 2012

Cheki Video ya Mchezaji Lionel Messi akiifungia Timu yake Barcelona na kuvunja Rekodi ya tangu Mwaka 1972 ya Straika wa Ujerumani Gerd Muller ya kufunga Bao 85 ndani ya Mwaka mmoja wa Kalenda kwa yeye kufikisha Mabao 86.

Lionel Messi  Rekodi
Supastaa Lionel Messi akiifungia Timu yake Barcelona Bao mbili na kuipa ushindi wa Bao 2-1 dhidi ya Real Betis  kwenye mchezo wa LA LIGA  na kumfanya  yeye akivunja Rekodi ya tangu Mwaka 1972 ya Straika wa Ujerumani ,Mchezaji  Gerd Muller ya kufunga Bao 85 ndani ya Mwaka mmoja wa Kalenda kwa yeye kufikisha Mabao 86 na wakati huo huo Straika hatari wa Atletico Madrid Radamel Falcao akipiga Mabao 5 katika Mechi moja walipoifunga Deportivo La Coruna Mabao 6-0.

 

WAFUNGAJI BORA


-Lionel Messi  Bao 23



-Radamel Falcao  16



-C.Ronaldo  13






Gerd Muller akijaribu

kufunga mbele ya

ukuta wa Uholanzi

 katika  World Cup

final ya 1974
Gerd Muller alifunga mabao 85 katika mechi 60 akiichezea Bayern Munich na Ujerumani Magharibi mwaka 1972 - rekodi ambayo imekuwepo kwa miaka 40  sasa.

 

Hivi ndivyo Muller alivyojitengenezea rekodi yake.


BAYERN MUNICH


Bundesliga: Mabao 42 katika mechi 34

European Cup: Mabao 10 katika mechi 4

Cup Winners Cup: Bao 1 katika mechi 2

DfB Pokal: Mabao 7 katika mechi 6

DfB Ligapokal: Mabao12 katika mechi 5 



GERMANY


Euro1972: Mabao 5 katika mechi 4

Mechi za kirafiki: Mabao 8 katika mechi 3


Kipindi bora kabisa cha ufungaji: Mabao 16 katika mechi 8
Muda mrefu bila kufunga: Mechi 3 


Katika magoli yote 85 aliyofunga - alifunga yote bila mkwaju wa penati.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad