Mkurugenzi
Mtendaji wa
LHRC, Dk Helen Kijo-Bisimba
|
Kituo hicho
kimesema vyanzo vingine vya raia kukosa haki zao za msingi za kuishi ni pamoja
na ajali, adhabu ya kifo, mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, mauaji holela
yanayofanywa na vyombo vya usalama.
Hayo
yalibainishwa jana jiji Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk Helen
Kijo-Bisimba, alipokuwa akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya miaka 64
ya Ttamko la Haki za Binadamu Duniani na miaka 10 ya uandishi wa ripoti za haki
za binadamu Tanzania.
Alisema
ripoti mbalimbali zilizoandikwa na kituo hicho tangu mwaka 2002, zinaonyesha
kuwa mauji ya raia yanayofanywa na vyombo vya usalama, yameongezeka kwa kasi na
kufikia vifo 193.
Alisema LHRC
wakati inaanza uandishi wa ripoti mbalimbali za haki za binadamu ikiwa pamoja
na haki ya kuishi, imebaini kuwapo kwa ongezeko kubwa la mauaji ya raia, jambo
ambalo si jema kwani linaondoa misingi ya haki za kuishi kwa binadamu.
“Mwaka 2002
hakukuwa na mauaji yaliyo ripotiwa lakini mwaka 2004 watu nane waliuawa na
polisi huko Mbeya, Musoma, Tarime na Dar es Salaam,” alisema Dk Bisimba.
Alisema
mauaji hayo yaliendelea na kwamba mwaka 2005 watu 36 waliuawa. Alisema mwaka
2006 watu wengine 37 waliuawa na kufuatiwa na mwaka 2007 ambapo watu 14
waliuawa. Dk Bisimba alisema licha ya mauaji yanayofanywa na polisi, tafiti
zinaonyesha kwamba pia kuna mauji yanayofanywa na raia wanaojichukulia sheria
mkononi.
“Katika
kipindi hiki cha miaka 10, tumebaini sababu mbalimbali lakini kubwa mbili ni
wananchi kukosa ulewa wa masuala ya haki za binadamu na sheria, jambo
linalosababisha kuamua kujichukulia sheria mkononi,” alisema.
Dk Bisimba
alifafanua kwamba miaka inavyo zidi kwenda taarifa mbalimbali zinaonyesha
kwamba watu wengi wanaendelea kupoteza maisha kutokana na jambo hilo.
No comments:
Post a Comment